Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

SHAMRA NA VIFIJO MITAA YA KENYA BAADA YA MAHAKAMA KUU KUTENGUA MATOKEO YA UCHAGUZI... TAZAMA PICHA ZA WAFUASI WA ODINGA...

Jaji Mkuu David Maraga ameagiza: Uuchaguzi wa urais uliofanyika 8 Agosti, 2017, nchini Kenya haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo matokeo yake ni batili.
"Natangaza hapa kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa.
"Agizo linatolewa, kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika kipindi cha siku 60."

Mgombea urais wa upinzani Raila Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika.
Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais.
Imetoa mfano mwema.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."
Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka amesema mahakama imekuwa mfano mwema kwa Afrika na dunia nzima.
"Ninajivunia kuwa Mkenya leo," amesema.
"Sasa tutaangalia kina kuhusu tume ya uchaguzi. Hatuan imani kwamba wanaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki." Alisema Kalonzo Musyoka.

Naye Wakili mkuu wa Bw Odinga, James Orengo, amesema mahakama imefuata katiba kubatilisha uchaguzi wa urais.

Amesema anatumai tume itaandaa uchaguzi wa marudio kwa njia huru na ya haki.
"Desturi ya kutoheshimu sheria lazima ikomeshwe na wahusika waadhibiwe. Mwaka 2013, maafisa wa tume ilibainika kwamba walifanya makosa. Tume imo mashtakani. Kabla tufanye uchaguzi mwingine, tume lazima ichunguzwe. Sidhani tutakuwa na tume hiyo ikiandaa uchaguzi tena."


Shamra shamra na vifijo vimetanda mitaa yote ya Kenya kwa wafuasi wa Odinga.


Mitaa ya Nairobi na Kwingine wafuasi wa Raila Odinga wamejazana kushangilia tamko la mahakama kuu.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top