Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

GAZETI LA TANZANIA DAIMA LAFUNGIWA NA SERIKALI KWA SIKU KADHAA


Serikali imelifungia Gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Kampuni ya Free Media Limited (FML) kwa kipindi cha siku 90.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abbasi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika, “Serikali imelichukulia hatua za kisheria gazeti la Tanzania Daima kwa mwendelezo wa kuandika habari za uongo… Taarifa kamili inakuja.”

Ingawa mpaka habari hii inawekwa katika mtandao, Dk Abbasi ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali hajabainisha ni hatua gani wamechukua, uongozi wa Tanzania Daima umesema wamefungiwa kwa siku 90.

Kaimu Mhariri wa gazeti hilo, Martin Malera akizungumza na Mwananchi amesema, 

“Tumepokea barua ya kulifungia gazeti letu saa 9:36 alasiri, barua ambayo imesainiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.”

Tanzania Daima limekuwa gazeti la tano kufungiwa katika kipindi cha miaka miwili likitanguliwa na Mwanahalisi, Raia Mwema, Mseto na Mawio ambayo yapo kifungoni kwa vipindi tofauti.

USIKOSE KUANGALIA MAMBO YA NACY FASHION HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top