IKIWA ni miaka miwili imepita tangu aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Haule Filikunjombe afariki dunia, mke wake Sarah Habiba amesema Tanzania ina pengo kubwa kwa kumpoteza Deo.
Katika ukurasa wake wa instagram, Sarah Habiba ameandika ujumbe huo, huku wakiadhimisha miaka miwili ya kifo chake kwa kufanya ibada takatifu.
“Mume wangu leo umefikisha miaka miwili tangu upatwe na mauti, kiukweli umeacha pengo kubwa kwa watanzania, jamii na familia kiujumla, watoto wako wanakumiss sana, mimi mkeo, Mungu akulaze mahala pema peponi mpenzi wangu, ntakukumbuka daima mpenzi”, aliandika jana Sarah Habiba.
Deo Filikunjombe alifariki Octoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta iliyoanguka kwenye msitu wa hifadhi ya Selous akitokea Dar es salaam kwenda Ludewa, akiwa na rubani wake William Silaa ambaye ni baba mzazi wa Jerry Silaa, na msaidizi wa Deo Filikunjombe, Bwana Mkwera ambao pia walifariki dunia.
Deo Filikunjombe atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na juhudi alizozionyesha kwenye kamati ya Bunge kuibua sakata la Escrow akiwa na wabunge wengine, akiwemo rafiki yake wa karibu mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
ANGALIA VIDEO YA NANCY CLASSIQUE FASHION UJUWE SEHEMU SAHIHI YA KUPATA NGUO SAHIHI
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.