Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

NDEREMO NA VIFIJO KUJIUDHURU KWA MUGABE ZIMBAMBWE...

Katika dakika chache zilizopita , spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya kesho Jumatano.
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.
Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake 1980.Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake.
Ameongoza kipindi cha uchumi ulioanguka ambapo raia wamezidi kuwa masiki zaidi ya walivyokuwa 1980.
Hatua iliosababisha yeye kuanza kungatuliwa madarakani ni ile alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita.
Hatua hiyo iliyooonekana na wengi kama ya kutaka kumrithisha madaraka mkewe
Iliwaudhi viongozi wa jeshi ambao waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizi cha nyumbani.
Source: BBC Swahili

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top