Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

HUU NDIO WIMBO MAALUM MSIBA WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI... NI SIMANZI NA MAJONZI...

 

MRITHI WA MATONYA AMEKUSOGEZEA NGOMA MPYA KAALI... LINK IKO HAPA...

Ngoma kali mpya iliyotambulishwa leo, Mwimbaji wa Nyimbo za Bongo flavor aliyewahi kutamba na Ngoma kama Barua na nyingie Sule Mabling'a, ameibuka tena na kuachia ngoma kali ambayo imeanza kugusa masikio ya wasikilizaji na wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya, ngoma inakwenda kwa jina la KUDANGA.
Ngoma iko youtube tayari na inaendelea kufanya vizuri lakini pia maandalizi ya video yameshakamilika na siku yoyote video itaanza kuchukuliwa. ngoma imefanywa na producer Mo. kuwa wakwanza kuitazama hapo maana nimekuwekea Link

MAREKANI YAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.
Kwa mujibu wa takwimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.
Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.
Idadi kubwa ya maambuizi imekuja wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.
Rais Trump alieleza namna alivyosikitishwa na idadi ya maambukizi.
Naye makamu wa rais Mike Pence alisema kuwa vipimo vya corona virus vipo sasa katika majimbo yote 50 na zaidi ya watu 552,000 wamefanyiwa vipimo.
Bwana Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawafahamu idadi ya maambukizi yaliyopo China, "Hamfahamu takwimu ya maambukizi yaliyopo China."
Bwana Trump alikuwa amekosolewa kwa taratibu alizoweka mpaka ifikapo sikukuu ya Pasaka, April 12.
Mipango yake inaonekana kugonga mwamba baada ya siku ya Alhamisi , maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kuonekana kusambaa kwa kasi nchini mwake.
Siku ya Alhamisi alitangaza kuwa Wamarekani inabidi warejee kazini , nchi inabidi irejee katika hali yake ya kawaida mapema iwezekanavyo.
"Tunaweza kuchagua upande ambao hauna maambukizi sana na kuanza kuwajibika."
Aliongeza: "Watu wengi niliposema mrejee katika shughuli zenu, mlinielewa vibaya" naona waliachana na suala la kuwa mbali, kuosha mikono, kushikana mikono na kila kitu ambacho kilizuiwa.
Ufafanuzi zaidi alihaidi kutoa wiki ijayo.
Source: BBC Swahili

KIKWETE: VIONGOZI WA UPINZANI SIO MAADUI WA SERIKALI

Wito wa rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kwa vyama tawala barani Afrika kutowachukulia viongozi wa upinzani kuwa maadui na badala yake kuwafanya kuwa washirika wakuu umeungwa mkono na wengi.
Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Afrika Kuhusu uongozi bora na sheria uliofanyika mjini Johannesburg, Kikwete alitoa changamoto kwa vyama vya kisiasa barani Afrika kushirikiana.
Alisema badala ya kuuchukulia upinzani kuwa adui, wanafaa kuchukuliwa kuwa washirika katika kuimarisha demokrasia inayoheshimu sheria.
Kufuatia taarifa hiyo mchanganuzi wa maswala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha kikatholiki cha Ruaha Prof Gaudence Mpangala alinukuliwa na gazeti la The Citizen nchini akisema kuwa taarifa hiyo ya rais Kikwete inafaa kupongezwa.
Bwana Mpangala amesema kuwa ni muhimu kwamba taarifa hiyo inatoka kwa kiongozi mwandamizi katika chama cha CCM.
''Tunaunga mkono taarifa ya Kikwete. Kuna tatizo kubwa na tunahitaji kutafuta suluhu ya kukabiliana nalo" Bwana Mpangala alinukuliwa na gazeti la The Citizen nchini akisema.
Akaongezea: "...Kuendelea kuwanyima wapinzani haki ya kutekeleza wajibu wao ni sawa na kuwanyima raia haki zao kimaendeleo..."
Kwa mujibu wa gazeti hilo bwana Mpangala amesema kuwa matatizo mengi yanayokabili Afrika yanatokana na ukandamizaji wa sera za kidemokrasia.
Vilevile mwalimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Richard Mbunda amesema kuwa ushauri wa rais Kikwete unaonyesha kitu ambacho alikuwa akifanya katika uongozi wake wa miaka 10.
Akizungumza na The Citizen alisema: "...Tumefanikiwa pakubwa katika kukuza demokrasia na kuheshimu sheria katika miaka ya nyuma lakini sasa tunarudi nyuma...."
''Ni lazima turudi katika mwelelekeo unaofaa'', alisema akiongezea :hii tabia ya watawala kuwachukulia wapinzani kama maadui inaufanya upinzani kuitazama serikali kama adui wake''.
Naye mshirikishi wa muungano wa watetezi wa haki za kibinaadamu THRDC bwana Onesmus Ole Ngurumwa amesema kuwa taarifa ya rais Kikwete ni funzo kubwa kwa wanasiasa barani Afrika na husuaan Tanzania.
Amewataka viongozi wa zamani kujitokeza hadharani na kuliangazia tatizo hilo huku akiwashauri wapinzani kutoogopa kufanya mazungumzo na rais Magufuli ili kutafuta suluhu ya kudumu.
''Kenya ni mfano mzuri kwetu katika eneo hili.Upinzani unatumia uhuru wa kidemokrasia na imesaidia kuondoa hali ya wasiwasi mbali na kuimarisha maenedeleo''.alisema.
© Copyright MO Design
Back To Top