KUTOKA kwenye insta story ya Rapa Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameandika; “Yani kujifanyaga mnawapa magari ooh label kubwa alau mkishindwana mna wapokonya magari yenyewe tena wasanii kwa wasanii.
“Ndio mjifunze wasanii wapenda magari ya bure wakati mna vipaji na wakati mkikomaa mnaweza kununua ya kwenu kwa hela zenu coz muziki huu una hela huu ndio maana wao wanaweza hata kuwadanganya na hayo magari na kuwadhalilisha kwa kuwapokonya... hunijui limeboa soon napiga tour najinunulia ligari langu lingine likubwa,” ameandika Nay.
Unahisi, Nay amelenga wasanii gani au label gani ambao wanawapa magari wasanii wao na kuwanyang’anya?..
Huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu ambaye ni raia wa Australia Bryana likawa limevunjika kulingana na mfululizo wa post zake kupitia insta story yake.
Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa tu baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Kajala.
Mbali na hayo mwanamuziki huyo ametangaza kuachia wimbo wake mpya siku ya kesho unaitwa ‘Mwaka Wangu’
Mahusiano ya mapenzi ni mazuri na matamu sana pale unapokuwa na mtu sahihi katika mahusiano husika, lakini pia yanakuwa mabaya na machungu ya kuumiza sana moyo pale unapokutana na mtu ambaye sio sahihi katika mahusiano husika ambapo upelekea mpaka wengine kufanya maamuzi ambayo sio sahihi na kufikia kupoteza uhai.
Kuna habari ambazo zimekuwa zikizunguuka kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusu Mtu moja aitwaye Daniel Lizy alipokuta message za mbaya katika simu ya mke wake siku 7 tu baada ya ndoa yao kufungwa.
".. najisikia vibaya sana wakati huu, sijui inawezekanaje nikute message mbaya hivi kwenye simu yake wakati ni siku saba tu toka tufunge ndoa,.. na nilichukua simu yake kutaka kucheza game kwa bahati mbaya nikajikuta nimeingia kwenye ukurasa wa Whatsapp ndo nikakutana na haya mambo..." anasema Daniel.
Kulingana na taarifa hizo, kijana anayejulikana kwa jina la Kunle Luv ndo alikuwa anachati na mwanamke huyo Tola ambaye ni mke wa Daniel na alikuwa anamuuliza kwa alikuwa hapokei simu zake wakati Tola akimwambia kuwa alikuwa anafunga ndoa na alikuwa hayuko tayari kuendelea tena na mahusiano yao.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuwa Kunle hakuwa tayari kuachana naye na alikuwa tayari mahusiano yaendelee hata baada ya ndoa hiyom kitu ambacho Tola hayuko tayari kabisa kukifanya hivyo ikapelekea amtangazie dau, yaani aamwambie ni kiasi gani cha pesa alitaka ili tu mahusiano hayo yasitishwe, lakini Kunle alikataa pesa na kutaka mahusiano yaendelea.
Massage zote hizo Daniel alikuwa akizisoma kwenye simu ya mke wake mbichi kabisa ambaye ametoka kufunga naye ndoa wiki moja tu imepita, yaani alihisi moyo wake kupasuka na asijue cha kufanya.
katika siku zote za uchumba wake na mwanamke huyo kumbe Tola alikuwa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa anajivinjari naye wakati huku kwa Daniel akipanga mipango ya ndoa,.. hii kweli ni hatari sana.
kama wewe ni Daniel utafanya maamuzi gani?.. Au ni ushauri gani ambao unaweza kumpa Daniel kama unapewa na fasi ya kumshauri?..
Jina lake ni Andiswa Selepe, Binti mwenye umri wa miaka 17 tu lakini amekuwa maarufu na mwenye kutamaniwa na kila mwanaume kutoka pande mbalimbali za Afika na dunia.
Andiswa Selepe ni binti mdogo anayetokea Mpumelanga, Mbombela South Africa, amekuwa maarufu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii hasa Instagram na Youtube ambako anamiliki account.
Accounts zake zimekuwa zikijizolea mashabiki wengi sana, ambapo picha zake zenye mvuto zimekuwa zikipata liks nyingi sana na comments za kumwaga ambapo comments nyingi ni za wanaume wanaokuwa wakimtaka kimapenzi. hii ni kutokana na uzuri wa sura yake na umbo lake zuri alilojaaliwa na Mwenyezi Mungu
Andiswa amekuwa ni Model mdogo na mwenye mvuto anayezifanya acounti zake zisheheni followers kwa ajili ya mwonekano na mvuto wake unaowaweka wanaume wengi katika hali ya kutamani kumnasa.
Amekuwa ni miongoni mwa warembo wengi wanaoifanya mitandao ya kijamii kutembelewa sana na wanaume hasa mtandao wa Instagram.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiendelea ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Mwandishi Wetu
UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo.
Mastaa mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo.
ILIANZA HIVI
Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí waliokuwa wakiwakodolea.
Kwa kuwa Diamond alikuwa host (mwendeshaji) wa shughuli hiyo, Lulu alikuwa akimwaga mauno huku akimshangilia Diamond kufuatia muziki wake wa nguvu uliokuwa unarindima ukumbini humo.
Kutokana na hali hiyo, Lulu aliendelea kucheza zaidi kwa madai kwamba anaupenda mno muziki wa Diamond hasa ulipodondoshwa ule wa Mdogomdogo.
Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zari.
WAONESHANA MAHABA
Ilifika wakati Diamond alionekana akimpiga Lulu busu mdomoni huku watu wakishangilia ëoyoooí lakini wao hawakuwa wakijali chochote kwani waliendelea kufanya yao.
Kuna wakati walikuwa wakitaniana na kucheka huku wakigongesha glasi zao za mvinyo na kukumbushana mambo mbalimbali ya siku za nyuma.
Baadhi ya watu walisikika wakisema kwamba, Lulu anamchokonoa mama Tiffah ‘Zari’ kwani kwa usiku huo yeye alikuwa tu nyumbani akinyonyesha wakati baba mtoto wake akijiachia na kimwana huyo.
“Naona Lulu anatafuta matatizo kwa Zari kwani mahaba wanayooneshana hapa ukumbini siyo ya kawaida, yaani hawa mastaa wetu mbona majangaaa,” alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa shughuli hiyo iliyokuwa ya kistaa kwani hakukuwa na ‘watoto wa mbwa’.
ONA VIDEO HII TOKA AYO TV
SHETTA AMWAGA FEDHA
Katika sherehe hiyo ilipambwa na mastaa kibao wa fani mbalimbali na mapedeshee wa mjini, walimmwagia Rommy mvua ya fedha huku mwanamuziki, Nurdin Bilal ‘Shetta’ akimzawadia fedha taslimu Sh. milioni moja ambapo shughuli iliendelea hadi majogoo.
Wakati hayo yakitendeka mmoja wa marafiki wa karibu wa Zari alimtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) kumfahamisha juu ya tukio hilo.
MASTAA KIBAO
Ukiacha Lulu na Shetta, baadhi ya mastaa wengine waliojiachia vya kutosha ni pamoja na Aunt Ezekiel na baba mtoto wake, Moses Iyobo, dada wa Diamond, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ sambamba na Juma Musa ‘Jux’, Hamad Ally ‘Madee’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na wengine kibao.
LULU ANASEMAJE?
Akizungumzia hali hiyo, Lulu alisema kuwa ilikuwa ni pati na kupiga picha na Diamond haikuwa ishu kubwa kwani ni watu wengi waliopiga naye picha.
“Siamini wala sihisi kama Zari anaweza ‘kumaindi’ ishu kama hiyo. Kama akimaindi atakuwa na lake jambo,” alisema Lulu.
TUJIKUMBUSHE
Kabla ya tukio hilo, Lulu aliwahi kudaiwa kutoka na Diamond lakini alikanusha vikali ishu hiyo huku akionesha kuwa jamaa huyo hana ubavu wa kumsogelea wala kufaidi penzi lake.