Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

JAMANI HOUSE GIRL WANGU HUYU ANANITAFUTA UBAYA HEBU NISAIDIENI... SOMA HAPA...


Jamani naomba ushauri kuhusu hili.

Mimi ni mume wa mke mmoja na watoto wanne. Hivi karibuni tumepata housegirl mpya kutoka Singida, amemaliza form four hakubahatika kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa sifa za shule za serikali. 
 
Ni mzuri wa kawaida, yaani hana muonekano ule wa mahousegirl-naamaanisha muonekano choka mbaya kweli anafaa hata kuwa mke wa mtu.
 
 Katika historia yangu sijawahi hata siku moja kutembea na housegirl na mpaka sasa nishaajiri hao h/girl si chini ya 6, huwa niko very serious na sitaki mazoea nao hata kidogo.

Huyu amekuja naona anataka kuniangusha katika msimamo wangu huu. Siku ya kwanza kutambulishwa kwake alionekana kushituka sana ingawa na mimi kwa ndani nilimkubali kuwa mzuri. 
 
Maisha yakaendelea na siku zikafunguka. Sasa toka siku hiyo amekuwa anakosa sana confidence(Ujasiri)  ninapokuwa nyumbani, mara atajikwaa, mara ataogopa kuja mbele yangu n.k 
 
Mbaya zaidi ninapokuwa peke yangu mfano wengine wapo mbali ananichangamkia sana na kutabasamu muda wote kila nitakalooongea yeye anatabasamu hata kama si la kufurahisha.
 
Nikimtuma kitu ataniletea wakati napokea anainua kichwa kuniangalia kiuchokozi halafu anatabasamu, basi na mimi nikawa natabasamu. 
 
Ikitokea labda nimerudi nyumbani na nahitaji chakula mapema atanipikia vizuri sana wakati mwingine anongeza kitu ambacho hakikupangwa kwenye ratiba ya chakula cha siku hiyo, anaweza kunkaangia mayai au akachemsha chai ya maziwa akaweka na viuongo haraka haraka na kunipatia chakula.

Tatizo, mke  wangu  keshashitukia hizo nyendo zake, amekuwa kila mara ananiuliza kuhusu mtu huyu, anasema mbona fulani ukiwepo anakuwa hana confidence nikamwambia mi sijui embu muulize alipomuuliza akamjibu wife kuwa eti ananiogopa kwa sababu aliambiwa na mlinzi mi ni mkali sana achunge asinikorofishe.
 
Lakini ukiangalia mapozi yake kwangu si ya mtu anayemuogopa. Siki hizi ameongeza zaidi, kunisalimia/kuniamkia kwake imekuwa ngumu sana ni mara moja moja sana.
 
Mi kwa ujumla ni mtu nisiyejali vitu vidogo vidogo na nilichojaribu kufanya ni kuwa mbali nae, nimeongeza kuwa serious, na wakati mwingine nakuwa mkali ninapoongea nae ili awe mbali nami au afute hicho anachofikiri au kukitafuta, Lakini nahisi ananitafuta ubaya.

Nimfanyeje? au nifanye lakini nahisi kujidhalilisha kwa mah/girl!

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top