Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

"MAM'DOGO LISA " SEHEM YA 2

ILIPOISHIA

 Alipofika, alimkumbatia mama yake kisha akamuuliza kwa upole.
"... mama, kuna kitu chochote ulichoongea na baba kuhusu kuoa?..."

SASA ENDELEA...

mama yake alimtazama mwanae kwa macho ya huruma na huku machozi yakiendelea kumchuruzika. "... sikia mwanangu, haya mambo ni makubwa sana kwako, na hayakutakiwa kujulikana kwenu, lakini ukweli ni kwamba yote mliokuwa mnaongea na baba yenu pale sebuleni nilikuwa nayasikia..." mama yake alinyamaza kidogo, akajifuta machozi kwa kutumia kitenge alichokuwa kajifunga kiunoni kisha akaendelea.
"... baba yenu sasa hivi amebadilika kwa kiasi kikubwa sana, na mabadiliko yake yanatokana na mwanamke aliyempata huko sijui wapi..." aliendelea kuongea Bi. pauline.
"... ina maana mama unajua kuwa baba anaye mwanamke mwingine?.. alihoji Denis.
"... najua, ila simjui huyo mwanamke, lakini kila siku baba yenu anamuongelea na kuniambia kuwa anataka kumuoa kabisa... aliongea Bi Pauline.
"... kwa hiyo wewe umemkubalia kuoa mwanamke mwingine na uzee wake wote ule?.." aliendelea kuhoji Denis. Bi. pauline alimtazama machoni mwanaye wa mwisho kisha akamwambia.
"... hiyo ndio sababu ya ugomvi wetu wa kila siku, kwa vile mimi sijakubaliana na kitu hicho ila yeye analazimisha..."
"... kwa hiyo alivyosema pale kuwa alishaongea na wewe na mlishayamaliza alikuwa anatudanganya? aliuliza Denis kwa mshangao.
"... na hicho ndicho kinachonitoa machozi kuona ni jinsi gani huyu mzee amebadilika mpaka kuamua kuwadanganya wanaye ili tu afanikishe lengo lake...? aliendelea kuongea Bi. Pauline kwa Huzuni. Denis aliinamisha kichwa chini kwa masikitiko kisha bila kuongeza neno aliondoka na kuingia chumbani kwake na kwenda kujitupa kitandani. kichwa kilimuuma kwa mawazo, alifikiria ni njia gani aitumie ili kumsaidia mama yake kipenzi, maana kaka zake wote walishaondoka, na mtu pekee aliyebaki kumsaidia mama yao ni yeye tu. kaka zake walijaribu kumsaidia mama yao kwa maneno ila yeye alihitaji kufanya kitu, na ni kitu hicho kilichokuwa kinamuumiza kichwa. afanye nini ili baba yake abadilishe mawazo ya kuoa na aendelee kuishi na mkewe kwa amani kama ilivyokuwa zamani. alikaa pale kitandani kwa muda mrefu akijaribu kufikiria mpaka usingizi ukampitia bila kupata muafaka wowote utakaomnusuru mama yake. alipokurupuka ilikuwa tayari giza limeingia. mwenyewe alijishangaa na hakujielewa ilikuwaje mpaka akapitiwa na usingizi.
alijiinua kitandani na kutoka taratibu mpaka sebuleni ambapo alimkuta baba yake akiwa amekaa huku akiangalia tv. hakumsemesha chochote ila alikaa tu akimtazama kwa makini mpaka baba yake akijishtukia kuwa alikuwa akiangaliwa. akamgeukia na kumuuliza
"... denis, una nini?.."
Denis hakujibu kitu ila kuendelea kumuangalia tu na kulijibu swali lake kwa kutingisha kichwa akimaanisha kukataa.
"... sasa mbona umefika umekaa kimya tu na kuanza kuniangalia, unafikiria nini?.."
aliuliza tena mzee Bisu huku akijiweka sawa kwenye kiti akimuangalia mwanaye.
"... sina la kusema baba, na siwezi kuwa nalo kwa sababu ya mawazo niliyonayo kichwani kwangu..." "... mawazo ya nini tena mwanangu?, unahitaji pesa?.."
Denis alimuangalia baba yake mzee Bisu kisha akamjibu.
"... sihitaji pesa wala kitu chochote, ninachokihitaji ni amani ya mama yangu tu basi..."
mzee Bisu alimuangalia mwanaye kisha bila kuongeza neno akainuka na kuondoka zake kuelekea chumbani, lakini kabla hajaingia akageuka kumuangalia mwanaye kisha akamwambia.
"... kama na wewe unataka kufuata mkumbo wa kaka zako, utahama hapa..."
Denis aligeuka na kumuangalia baba yake "... mimi kuondoka hapa nitaondoka, ila ni baada ya kuhakikisha mama yangu anaishi kwa furaha ka ilivyokuwa zamani..."
aliongea Denis huku naye akiinuka. mzee bisu alimtazama kwa jazba mwanaye huyo mdogo na kuanza kumsogelea taratibu.
"... una maanisha kuwa unataka kupambana na mimi?..
alimuuliza huku akiendelea kumsogelea lakini Denis hakusimama alipoinuka alianza kuondoka kurudi tena chumbani kwake na kabla hajaingia akamjibu baba yake.
"... siwezi kupambana na wewe baba, wewe ni mzazi wangu ila najua mwenyewe nitafanya nini kumnusuru mama yangu..."
alimalizia kisha akaingia chumbani kwake na kujifungia mlango.
ITAENDELA IJUMAA, USIKOSE KUFUATILIA KISHA HIKI CHA KUSISIMUA.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

3 Maoni

figaro..kazi nzuri komaa kaka

Reply

umeonaeeeee.... nipeni support... nyie ndo wa kali wangu...

Reply

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top