Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAM'DOGO LISA SEHEMU YA 7

MO

ILIPOISHIA SEHEMU YA 6 ...

Nikimkubalia huyu mzee kama alivyosema ataninunulia kila alichokiahidi.. ... lakini kutemabea na mzee mtu mzima kama huyu si sawasawa na kuytembea na baba yangu?... hapana... mungu wangu nifanye nini sasa mimi..."

SASA ENDELEA NA SEHEMU YA 7

aliendelea kuwaza Hasina. lakini ghafla aligutushwa toka mawazoni na mkono wa mzee Bisu uliomshika ghafla na kisha kuanza kumvuta kuelekea chumbani kwa kwake, yaani chumbani kwa Hasina mwenyewe. Bila kujielewa na kama vile alikuwa ametokwa na fahamu, Hasina alijikuta akimfuata mzee Bisu kama mbuzi apelekwaye machinjoni bila kujijua kuwa anakwenda kuchijwa.
Ni kama tayari alikuwa amekubaliana na ombi la mzee Bisu bila yeye mwenyewe kujijua kuwa alikuwa tayari kwenda kufanya kile walichotaka kwenda kukifanya au la. waliongozana mpaka mlangoni kwa chumba cha Hasina huku mzee Bisu akiwa bado kamshikilia mkono.
Mzee Bisu aliusukuma mlango ambao haukuwa umefukwa kisha akamtanguliza Hasina kuingia ndani ya chumba hicho kisha na yeye akawa anafuata nyuma huku akiangalia huku na huku kama kuna mtu ambaye alikuwa akiwaona. lakini kabla hajafingia kabisa mzee Bisu alisikia sauti kama ya mtu ikiongea nje, alisimama ghafla na kuanza kusikiliza kwa makini ile sauti ni ya nani na ilikuwa ikitokea upande gani. Mle chumbani Hasina naye alisimama na kuanza kumkodolea yule mzee macho. alijiuliza ni kitu gani kimetokea mbona mzee amesimama ghafla. ni kweli kuna mtu alikuwa akiongea nje ya nyumba hiyo, au tuseme kuna watu walikuwa wakiongea nje ya nyumba hiyo. aliposikiliza kwa makini. mzee Bisu aligundua kuwa ilikuwa ni sauti ya mke wake lakini hakujua alikuwa akiongea na nani. haraka sana akarudisha kichwa mle chumbani na kumuangalia Hasina ambaye naye alikuwa akimkodolea macho.
"... Hasina, mambo yalisha haribika... sasa sikiliza kesho asubuhi ntaenda kununulia vile vitu kama nilivyo kuahidi sawa?.."
Hasina aliitikia kwa kichwa.
"... nafanya hivyo kwa vile ulishanionesha moyo wa kunikubalia... sasa kesho saa nne asubuhi wakati unakwenda sokoni, utanikuta kwenye kile kibaa cha pale kwa Mangi sawa?.."
aliendelea kuongea haraharaka mzee bisu kabla mkewe hajaingia na kumkuta chumbani kwa Hasina. "... kwani baba wewe kesho huendi kazi?.." Hasina alijikuta akipata ujasiri wa kuuliza swali.
"... kazini ntaenda lakini ntatoka mara moja ilitwende nikununulie nilichokuahidi alfu ntarudi tena kazi..."
"... sasa ukirudi si uje unichukue hapa ndio twende?.."
"... nilisakuambia sitaki mtu yeyote ajue kuwa mimi ndo nnaye kununulia hivyo vitu, kwa hivyo nikija hapa kukuchukua kila mtu atajua..." aliemalizia mzee Bisu kisha akachungulia mlangoni haraka, hakuona mtu, akamgeukia tena Hasina.
"... tumeelewana?..."
"... ndio...`'
"... hakikisha unafika pale mapema ilituwahi kwenda na kurundi sawa?.."
"... haya..." alijibu hasina. mzee bisu hakupenda kupoteza muda tena pale. alitoka haraka akaelekea kwenye sofa lake alilokalia mwanzo akakaa nakuendelea kufuatili vipindi kama kawaida. ilikuwa kama bahati yake kwani kitendo cha kukalia sofa tu na mlango ulifunguliwa ambapo mke wake aliingia. yaani kama angeongeza sekunde mbili za kuongea na Hasina mkewe angemfuma.
Alipoingia ndani Mkewe alishituka kukuta kuwa mumewe tayari amerudi, maana huwa sio kawaida yake kurudi mapema kiasi kile.
"... heh, mume wangu, tayari umerudi?... leo mbona mapema hivyo?.." alihoji Bi. Pauline huku akimsogelea mumewe na kwenda kukaa jirani yake.
"... ah... nimewahi kurudi leo nimeisi uchovu... ulikuwa wapi?.." alijibu kisha akaunganisha na swali, alikuwa akijaribu kujiweka sawa asioneshe ule wasiwasi aliokuwa nao.
"... wala hata sikuwa mbali... nilikuwa hapo kwa mama ole..."
Mzee bisu hakupenda kuuliza swali jingine alinuka na kuingia zake chumbani ambako alijiandaa na kwenda bafuni kuonga. huku nyuma mkewe alianza kumuita hasina.
"... hasina,.. we Hasina..." "... bee mama... aliitikia kwa sauti Hasina huku akitoka chumbani kwake na kuelekea pale alipokuwa Bi. Pauline. hakuwa katika hali yake ya kawaida, alijihisi kumuogopa Bi. Pauline japo hakuona kosa alilolitenda, kile kitendo cha kuomuona sungura wa Mzee Bisu akiwa katuna ndani ya Nguo aliyovaa ukiongeza na ule udadisi wa yule mzee kutaka kuvunja naye amri ya sita, ni kama vilimtia wasiwasi kidogo, lakini hata hivyo alijikaza kisabuni na kwenda mpaka pale alipokuwa akiitwa na Bi Pauline.
"... mbona umejifungia peke yako chumbani, kuna nini?.." alihoji Bi. Pauline.
"... hanmna kitu mama nimekaa tu..." alijibu Hasiina huku akitazama pembeni, hakuwa tayari kumtazama Bi. Pauline machoni, mwenye hata hakujielewa ni kwanini lakini ilitokea tu.
Bi. pauline aliingiza mkono ndani ya sidiria yake akatoa noti ya shilingi efu mbili na kumpa hasina.
"... nenda pale dukani kaniletee panadol, nahisi kama mwili wangu umechoka sana..."
bila kuongea neno Hasina aliipokea ile pesa na kutoka.

************************************


Saa tatu asubuhi, mzee bisu alikuwa akikamilisha baadhi ya vijikazi vidogo vidogo vilivyokuwa kwenye meza yake, alikuwa akivifanya kwa harakaharaka ili awahi kutoka, na mda wote alionekana kama mwenye furaha sana kitendo ambacho hata secretari wake alikishitukia lakini hakuweza kumuuliza kitu. kazi zilizobakia aliamua kuziacha na kujiahidi kuwa atakuja kuzimalizia atakaporudi.

Hasina alikuwa amemaliza kazi zote za asubuhi za pale nyumbani, alikuwa sasa akijiandaa kwenda sokoni....

ITAENDELEA.... USIKOSE SEHEMU YA 8

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top