Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ALLY CHOKI AONGEZA NGUVU EXTRA BONGO


CAMARADE ALLY CHOKI (Pic: MODesign)
Kiongozi wa Bendi mahiri ya Muziki wa Dansi nchini Tanzania Camarade Ally Choki, jumapili amewatangaza wacheza show wapya katika Bendi hiyo na kuwanadi kuwa ni moto wa kuotea mbali.
Ally Choki amesema kuwa wacheza Show hao wamejiunga rasmi na Bendi na kila wanapofanya Shoow watakuwa wakionekana.
"... Nimeongeza wachezashow wapya ili kuongeza nguvu katika safu hiyo ya wacheza show wakike, unajua mashabiki wanapenda kuona vitu vipya na mambo mapya..." alisema Ally Choki.

WACHEZA SHOW WAPYA WA EXTRA BONGO (Pic: MOD esign)
Aliendelea kusema kuwa Jumapili Ijayo, atatangaza waimbaji wapya watakaojiunga rasmi na Bendi. alipohojiwa ni waimbaji gani watajiungana Bendi hiyo, alikuwa na haya ya kusema.
"... kusema kweli siwezi kuwataja ni wanamuziki gani wanajiunga na Extra Bongo Jumapili hii, ila nawaomba tu wapenzi wa Extra Bongo waje wajionee wenyewe..."
Choki amesema kuwa kilaJumapili wanakuwepo Hapo Garden Breeze Mgomeni Hospitali.
MMOJA KATI YA WACHEZASOW WAPYA WA EXTRA BONGO (Pic: MODesign)

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top