Kwa mujibu wa Uongozi wa Muziki Nchini Marekani unaomuongoza Msanii wa muziki wa R & B Chriss Brown, ulietoa taarifa kwa uongozi wa muziki Tanzania unaomuongoza Msanii wa Bongo fleva Ali Kiba msanii ambaye yuko chini ya uongozi wa kampuni za Sumsung.
Kwa taarifa ziliopo katika mtandao VIP Beats nchini Marekani, zinaeleza kuwa tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka 2014, Uongozi wa Msanii Chriss Brown ulipokea taarifa ya maombi ya muungano wa wasanii wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya Ali Kiba na Chriss Brown, maombi hayo yaliambatanishwa na soft-copy zilizobeba nyimbo tatu za Ali Kiba ikiwemo Single Boy, Mwana pamoja na wimbo aliofanya katika Project ya ONE 8.
Uongozi wa Criss Brown ulithibitisha kupokea maombi hayo na ulionesha kupenda sauti ya Msani Ali Kiba na kutoa tamko kuwa uko tayari kisimamia kazi ya pamoja itakayofanywa na wasani hawa.
Kwa Upande wake Chris Brown alisema hana tatizo yuko tayari kushirikiana Ali Kiba kwani alipata nafasi ya kutazama Projecy ya one 8 na aliona kiwango cha Ali Kiba kinaridhisha japokuwa anahitaji marekebisho madogo sana.
Lakini kumekuwepo hali ya mshangao kwanini dili hili linachukuwa muda mrefu bila kufanyika. lakini baada ya uchunguzi imebainika kuwa huenda uongozi wa Chris Brown umeingia mashaka kufanya nyimbo na Ali Kiba baada ya kubaini kuwa kuna Msanii mwingine Tanzania anayeitwa Diamond na anafanya vizuri Afrika kwa sasa.
"... hapa lazima kuna mkono wa Diamond, kule kwenda kwake Marekani katika zile tuzo za BET kunaonekana kumchanganya sana Chriss Hivyo kushindwa kuwa tayari kufanya nyimbo na Ali Kiba kwanza... I see kama ni kweli Diamond atakuwa amempotezea Kiba nafasi ya kupiga mamilioni ya pesa kama nyimbo hiyo na Chriss Brown ingetoka..." alisema mdau mmoja wa muziki.
Endelea kufuatilia Modesigntz Beste wangu wa ukweli, na mimi ntaendelea kukuwekea kila habari inayonifikia.
PIA USISAHAU KULIKE PAGE YETU ILI NA WEWE UWE MWANAFAMILIA NA HABARI ZETU ZIWE ZINAKUFIKIA MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.