Tasnia ya muziki Tanzamia imeingiwa na majonzi tena kwa kupotelewa na nguli wa muziki na baba wa Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva Prince Dully sykses, Mzee Abby Sykes.
Akiongea kwa majonzi ikiwa ni pamoja na kuelezea kitu kilichosababisha umauti wa baba yake, Dully Sykes ameanza kwa kusema >>’Mzee alikua ana vidonda katika miguu na ndiyo chanzo kikubwa, sumu ikasambaa ikasababisha kifo chake, vidonda vilishindwa kupona kwa ajili ya moshi wa sigara ila zaidi hakuwa na tatizo jingine lolote manake baba yangu alikua strong’
‘Alianza kuugua vidonda miezi minne iliyopita, miezi miwili alikua anavumilia tu lakini miezi miwili ya mwishoni ndiyo vilizidi kumsumbua, mazishi tunategemea kuyafanya February 16 2015 saa kumi jioni kwenye makaburi ya Kisutu lakini safari ya kwenda msikitini tutaanza saa 7 mchana‘ – Dully.
Marehemu Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba mzazi wa mwimbaji wa Bongo Fleva Prince Dullysykes, alifariki saa 8 mchana February 15 2015 akiwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Endelea kufuatilia modesigntz Beste wangu wa ukweli, na mimi ntaendelea kukusogezea kila habari inayonifikia.
PIA USISAHAU KULIKE PAGE YETU ILI NA WEWE UWE MWANAFAMILIA NA HABARI ZETU ZIWE ZIKIKUFIKIA MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.