Unaposema Kigoma ni mwisho wa Reli naamini kabisa unakuwa una maanisha kuwa Kigoma ni mwisho wa kila kitu.
Huyu hapa mwengine kutokea Mkoa huo kuja kuwa pinduapindua akina Diamond,Ali Kiba na Dimpoz.
TAFF CHUMA sio jina geni katika masikio ya wale wa penzi wa Bongo Movie, tukirudi nyuma kwenye Historia ya filamu za kitanzania utakutana na jina hili ambalo lilifanya vizuri sana na linaendelea kufanya vizuri katika Tasnia ya Filamu Bongo.
ukivuta kumbukumbu katika Tamthila ya Jumba la Dhahabu utakutana naye, Filam ya Mahabati, My Darling, Sikio la Kufa na nyingine ambapo na hivi karibuni ataonekana kwenye sinema kaali sana ya kitanzania iitwayo KINTU.
Ni mtu wa vipaji na kweli Kigoma ni mwaisho wa vipaji, Sasa ameugeukia muziki wakizazi kipya na anafanya vizuri, na kama huamini,
HII HAPA VIDEO YAKE...
Pamoja na kufanya filamu, pia kujikita kwenye muziki wa kizazi kipya, Taff Chuma mara nyingi anaonekana kwenye jukwa la Bend Kali ya Muziki wa dansi ya EXTRA BONGO, akiwa chini ya nguli wa muziki Camarade Ally Choki.
hapo ndipo utathibitisha kuwa kweli TAFF CHUMA anavipaji lukuki.
Endelea kufuatilia modesigntz upate uhondo zaidi, na mimi ntaendelea kukusogezea kila stori inayonifikia Beste wangu wa Ukweli...
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI UWE MWANAFAMILIA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.