Kuanzia magazeti, mitandaoni mpaka kwenye redio… kwenye mtiririko wa stori za mastaa wa Tanzania zilizoongelewa au kuandikwa sana ndani ya wiki 6 zilizopita, hii ya mwigizaji Aunty Ezekiel kuwa na ujauzito na dancer wa Diamond Platnumz aitwae Mose Iyobo imo kwenye orodha.
Wawili hawa walitajwa kuwa mapenzini kitambo na hata ujauzito wa Aunty iliandikwa kwamba baba kijacho ni Mose japo Aunty mwenyewe alikanusha.
Nakumbuka alisema ‘kuhusu taarifa za mimi kupewa ujauzito na Mose Iyobo, hizo taarifa mwenyewe nasoma kwenye magazeti nasikia kwenye Radio kama unavyosema lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani‘
Pamoja na kukanusha huko, wawili hawa wameendelea kuchukua nafasi kwenye vichwa vya habari kutokana na post zao wenyewe kwenye page za instagram wanazomiliki ambapo wiki mbili zilizopita Mose aliweka hii picha hapa chini huku Aunty akiwa juu yake kitandani na kuandika ‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila……..?
Kingine kilichokolezea imani za wengi kwamba wawili hawa wapo mapenzini kweli ni Post ya Aunty Ezekiel siku ya Valentine ambapo alipost picha ya Mose na kuandika ‘Happy Valentine Moo akee Baby akee boo boo wa mm baba akee………. Jaden, Baba wa…………… Umbea tyuuuu nimemaliza waone kwanza, Aunty akee lv u‘
Baada ya hii post ya Aunt, saa kadhaa baadae kwenye siku ya Wapendanao Mose alikolezea tena kwa kupost picha ya Aunty na mtoto na kuandika ‘Kabla siku haijaisha hawa ndio washikaji zang…… THEY JUST SAY MY DAD IS THE BEST’
Aunty Ezekiel aliolewa zaidi ya miaka miwili iliyopita, na anapoulizwa kuhusu ndoa yake anasema kuwa ndoa bado iko na itaendelea kuwepo kwani yeye hajaachika.
Endelea kuwa karibu na modesigntz, na mimi nyaendelea kukuwekea kila habari inayonifikia Beste wangu wa Ukweli.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KAMA BADO HUYAFANYA HIVYO ILI HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.