
Diamond Platnumz amewasihi wasanii wa Tanzania kuacha kulalamika
kutawaliwa na muziki wa Nigeria bali wanatakiwa kutoa ngoma kali kuwapa
ushindani.
Diamond alitoa kauli hiyo kwenye 255 ya XXL kupitia kituo cha redio cha Clouds FM.
“Unajua huwezi kuwalaumu tu Wanigeria, wao walitumia taaluma yao na
technique zao ili kuteka soko, sasa ukionekana unamind utaonekana pia
hauna akili ya kibiashara,” alisema.
“Cha muhimu nikuhahakikisha unatoa
nyimbo kali ambayo itasikika yako na kuifunika hizo za Nigeria.
“Tunatakiwa wasanii wa bongo kutoa ngoma kali ili mashabiki wapende
maana huwezi kumzuia Dj asipige nyimbo za Nigeria maana mashabiki
wanaomba inabidi na sisi tufanye hivyo ili uombwe muziki wetu zaidi.
Mfano zamani zilikuwa zinafanya vizuri nyimbo za Kongo lakini baada ya
kuanza kutoa ngoma kali sasa hivi huzisikii tena kama zamani.
"Inabidi
pia sasa hivi tufanye hivyo tusilalamikie ma Dj tu, naamini sasa hivi
muziki wa Tanzania umeshakua. Kinachotakiwa ni kuzuia soko la nje
lisiteke muziki wa Bongo kwa kutoa kazi nzuri zaidi,” alisisitiza.
BOFYA "LIKE" UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.