UKIWATAJA
chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa kwenye Bongo Fleva basi jina
la Mwanadada, Pamella Daffa a.k.a Pam D huwezi kuliweka pembeni
kutokana na wimbo wake wa Nimempata.
Wimbo huo ni wa kwanza kwake kufanya vizuri
na kumweka vema kwenye ramani, umetengenezwa na prodyuza Mesen Selekta
ambaye pia amemshirikisha kutoka Studio za D Fatality Music na umemuweka
kwenye nafasi nzuri ya kuchukua tuzo katika Tuzo za Kili
zitakazofanyika Juni, mwaka huu. Pam amezungumza na gazeti hili, hivi
ndivyo ilivyokuwa:
Unafanya nini kukuza muziki wako?Vipo vingi lakini zaidi nimeelekeza nguvu katika kujitambulisha mikoani na sehemu nyingine. Kingine ambacho nimegundua katika kuzunguka kwangu ni kuwa watu wengi wanaujua wimbo kuliko wanavyomjua msanii mwenyewe.
Mfano kuna siku tulienda Zanzibar kila kona wimbo wa Nimempata ukawa unachezwa lakini wakawa hawanijui.
Unalionaje soko la muziki?
Soko liko poa kwa levo yangu ambayo mimi nipo, nimeanza kupata shoo mpaka kuna nyingine nazipunguza kutokana na sababu tofauti.
Naamini nitachukua tuzo kwa kuwa Nimempata ni wimbo ambao umebahatika kuteka sehemu kubwa ya jamii ya muziki wa Tanzania.
Nje ya muziki unajihusisha na nini?
Wengi wanajua kuwa mimi ni mwalimu, hapana mimi ni MC nimekuwa nikifanya kazi zangu nyingi pale Dar Live, pia ni mtangazaji ingawa kwa sasa nina mpango wa kurudi darasani kusomea uandishi wa habari levo ya diploma.
Mpango wa kolabo na Mnigeria
Mpango huo upo ila kuna vitu vilikuwa hajikamilika, sitamtaja jina huyo msanii ni nani ingawa ana jina kubwa tu kwa sababu nataka kufanya kama ‘surprise’ kwa mashabiki wangu.
Uhusiano wako na Mesen upoje?
Tetesi zimekuwa nyingi kuwa tuna uhusiano wa kimapenzi lakini ukweli ni kwamba Mesen ni ndugu yangu kabisa wa damu, ni binamu yangu ambaye ni rafiki yangu pia wa karibu, ndiyo maana unaona tupo karibu sana kwa kuwa hata familia imekuwa ikitoa sana sapoti sana kuhusiana na sisi.
Baada ya Nimempata nini kinafuata?
Siyo kwamba nimetulia kinachoendelea ni kuwa sitakiwi kuwa na haraka ya muziki. Wimbo wa Nimempata bado unatamba sana kwa hiyo naupa muda uendelee kujitangaza zaidi, nisije nikautoa mwingine harakaharaka halafu nikauzima mapema Nimempata.
Kuna nyingine kali mbili nimeshazifanya zimekamilika, unasubiriwa muda tu ziachiwe hewani, moja nimefanya na Christian Bella na ndiyo utakaotangulia kutoka na video yake halafu utafuata niliofanya na Ya Moto Band.
BOFYA LIKE UJIUNGE NASI MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.