Kumezuka ghasia katika Mji wa Bujumbura nchini Burundi kati ya
maofisa wa polisi na waandamanaji wanaoishutumu serikali kwa kufanya
mapinduzi ya kikatiba.
Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi huku maofisa wa polisi wakilazimika kurusha mabomu ya machozi hewani.
Ghasia hizo zinafuatia tangazo la jana kwamba Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania muhula wa tatu wa urais.
Upinzani umeitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa katiba na kuonya kuwa huenda ikaathiri makubuliano ya amani ambayo yalimaliza miaka kadhaa ya mapigano ya kikabila.
Serikali imesema kuwa maandamano hayo si halali.
Maelfu ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa hilo katika majuma ya hivi karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi utakaofanyika Mwezi Juni mwaka huu.
BOFYA LIKE KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.