
HABARI: Daniel Micho Mulume, MO Design Congo DRC.
Mji wa Beni ni miongoni mwa Tarafa 6 za Jimbo la Kivu kaskazi mashari mwa Nchi ya DRC,
mji huo umegeuzwa kuwa uwanja wa vita na mauaji ya kinyama kwa muda wa zaidi ya miaka 20 sasa. Tasmini ya mwisho ya Shirika moja la kiraia jimboni humo lilitanabaisha kuwa ni zaidi ya watu 116 walishapoteza maisha katika mauaji hayo na maelfu ya raia wengine kupelekwa kusikojulikana ndani ya muda wa miaka 2 tu.
Mauaji hayo bado ya naendelea kufanywa na watu wanaodhaniwa kuwa ni waasi wa Uganda yaani ADF kwani mnamo tarehe 30 Mei watu wa 3 tena waliuawa katika Kijiji cha Kokola katika Tarafa hiyo ya Beni.
Mbunge wa Beni Juma Balikwisha alikuwa na haya ya kusema pale alipoutembela mji wa Goma.
"... Kulikuwa na shambulizi Kokola katika majira ya mchana kati, na kuna ujumbe tunao kwamba bado adui wanaendelea kuzunguka zunguka, hivyo tuna dhani kuwa kunashambilio lingine bado linaandaliwa..." alisema Juma Balikwsha (Mb)
Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa swala la usalama wa Beni liliwakutanisha wabunge wote wa majimbo hayo ikiwa ni pamoja na wale wa Kivu kaskazini kusitisha vikao vya Bunge tangu Tarehe 3 Mei ili kuiomba serikali kufanya hima katika kusimamia usalama na kusitisha mauaji hayo yanayoendelea Beni.
"... tuna maswali mengi ambayo tunajiuliza dhidi ya mauaji haya ya kinyama na hili kundi la ADF ambalo lilikuwa limetokomezwa. sasa kusema limezuka tena kuja kuteketeza Jeshi letu na vikosi vya usalama, ikiwa ni pamoja na kuchinja watu kinyama, je hii si vita kutoka nchi jirani?.. Ni muda tu tumetoka kwenye kikao ambacho kilituweka kwa masaa zaidi ya 7 ambapo tulikuwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Mazingira na Waziri wa Usalama, tumewahoji maswali mengi juu ya swala hili la haya mauaji ya kinyama na nini hatima yake kwani Jeshi linaonekana kuchoka kuwalinda raia?.. tumeambiwa tusubiri majibu ndani ya masaa 48.." alisema Juma Balikwisha (Mb).

Naye Kasonga Cibangu ambaye ni msemaji wa Jeshi la Taifa alikuwa na haya ya kusema.
"... Kaskazini mwa Jimbo letu, FARDC walifaulu kubomoa ngome ya waasi hao ADF katika kijiji cha Kokola kilicho umbali wa kilomita 30 toka ulipo Mji wa Beni.
Operesheni hizi zilifanyika katika Kitongoji cha Bambada katika Mtaa wa Ocha - Erengeti. Waasi wa 2 waliuawa na kukamata silaa za kivita. Katika operesheni hiyo watu watatu waliuawa na waasi hao walipokuwa wakikimbi, miongoni mwa waliouawa ni Waalimu wa 2 na Mkuli ma mmoja, hata hivyo Operesheni ya kuwasaka waasi hao bado inaendelea..."
alisema Msemaji wa Jeshi la Taifa FARDC.

Rais Joseph Kabila katika ziara zake 3 ambazo alishafanya katika Mji huo wa Beni, aliahidi kuwa atalimaliza tatizo hilo la mauaji lakini hadi leo watu wanaendelea kuuawa mbele ya vikosi vya Monusco.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.