Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

IKO HAPA YA BARAKA DA PRINCE KUMCHEZEA LINAH NYETI HADHARANI...


Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’ na Linah.
DAR ES SALAAM: Katika hali isiyo ya kawaida, staa wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Baraka Da Prince’ amenaswa akimdhalilisha staa mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kwa kumshika sehemu zake nyeti.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita katika Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na shoo ya kuadhimisha miaka kumi ya staa wa Muziki wa Dansi, Christian Bella ‘Obama’.
Baraka na Linah waliokuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye ratiba ya kuburudisha siku hiyo, walifanya tukio hilo walipokuwa nyuma ya jukwaa (back stage) walipokuwa wakisubiri muda wao wa kutumbuiza ufike.
Paparazi wetu aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.
“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.
Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.
“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.
Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.
Linah na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top