Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

WABUNGE WA UPINZANI WATOKA TENA NJE WAKIPINGA NAIBU SPIKA KUENDESHA BUNGE...

Wabunge wote wa vyama vya upinzani leo tena  wametoka nje kupinga Naibu Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge huku wakisema wanamwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Naibu Spika, Dk. Tulia.
Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge, wabunge hao wametoka nje  majira ya saa 3:00 asubuhi na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.
Kambi  upinzani  ilianza utaratibu huo juzi kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya Dk. Ackson kuingia ukumbini.
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, juzi alisema wataendelea kutoshiriki vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika hadi pale “haki itakapopatikana.”

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top