
Baada ya kimya cha mda mrefu ambacho kimepelekea mpaka mashabiki wake wengi kumsahau, mkali wa miondoko ya Hip Hop, Dooperman a.k.a BABA UBAYA, ameibuka tena katika anga za mziki huo na kuja na vitu vikali ambayo vinaonyesha kweli alikuwa anajipanga.
Akizungumza na MO Designtz Baba Ubaya amesema kuwa kimya chake hakikumaanisha kulikimbia Game bali alikuwa chimbo akijiweka sawa kwani mziki huu hauitaji kukurupuka kwani sasa hivi vijana wengi wanafanya vizuri, sasa ikitokea mkongwe anaharibu itaonekana kuwa amekwisha kazi yake.
"... Ukimuona Kondoo kainama ujue anatunga sheria, mimi ni mkongwe wa siku nyingi sasa kama nilikaa kimya sio kuwa nililikimbia Game, bali nilikaa pembeni kusoma game likoje lakini pia nilikuwa nafanya mambo yangu mengine..." Alisema Baba Ubaya.
aliendelea kusema kuwa Sasa ameachia ngoma mpya iitwayo TUMKUMBUKE MUNGU ambayo ndio inatamba kwenye vituo mbalimbali vya redio ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii kama vile Youtube, Facebook, Instagrame, Mkito .com na Mdundo.com.
amesema kuwa kabla ya ngoma hii ambayo pia anajiandaa kuifanyia Video, kuna ngoma nyingine alishaiachia iitwayo WAMENIMISS aliyomshirikisha T.I.D, na iko katika vituo vya Redio na Tv pia katika mitandao ya kijamii.
Baba ubaya amewaambia wapenzi na mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani huu ni mwanzo tu wa vitu vizuri
KUISIKILIZA, NGOMA IKO HAPA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.