Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

IDRIS ELBA KUIGIZA KAMA JAMES BOND KATIKA 007 MPYA


PRODUCERS  wa filamu za 007 James Bond, Barbara Broccoli na Michael G. Wilson wamethibitisha kuwa Jina la Idris Elba ni miongoni mwa majina yaliyotajwa wakati wanaongea kuhusu mwigizaji wa kuigiza kama James Bond baada ya Daniel Craig kumaliza filamu yake ya mwisho ‘No Time to Die’.

 

Hii ni filamu ya 25 ya James Bond. Majina mengine yaliyotajwa kwenye mazungumzo hayo ni Tom Hardy, Henry Cavill na Regé-Jean Page.

 

Oktoba 2021 Elba alisema hatachukua kazi hio ila kuna wakati alifikiria na alikuwa na shauku ya kuigiza kama 007 James Bond. Elba ameshaonyesha uwezo mkubwa wa kuigiza kupitia show kubwa za tv kama Luther, The Wire na filamu ya The Suicide Squad.

MO Designtz


 

DAVIDO NA WIZKID WAMALIZA BIFU


 WASANII wakubwa Barani Afrika na duniani, Ayodeji Ibrahim Balogun almaarufu kama  ‘Wizkid na David Adedeji Adeleke almaarufu kama ‘Davido’ wamemaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda na sasa hivi wakikutana ni amani kama inavyoonekana kwenye picha.

Hii imetokea jana baada nguli hao wa muziki barani Afrika kukutana club nchini Nigeria na kukumbatiana kwa furaha, jambo ambalo limeleta furaha kwa mashabiki wao pia kuona wakipatana tena na kuwa kitu kimoja.








KUTANA NA BINTU MREMBO ALIYEJIZOLEA UMAARUFU KUTOKANA NA UMBO LAKE...

 Hajia Bintu ndilo kjina lake, ni mrembo kutoka nchi ya Ghana aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia mitandao ya kijamii hasa mtandao wa Tik Tok kwa kuonesha umbo lake zuri lenye mvuto wa kipekee.

Bintu amekuwa akipost picha mbalimbali zinazoenyesha umbo lake na kusababisha kujipatia followers wengi na wengi wakisifia na kuvutiwa na umbo lake lilivyokuwa nzuri.


Warembo wengi wenye maumbo ya kuvutia wamekuwa wakijaribu kutupia picha kwa minajiri ya kutaka kushindana naye lakini bado Bintu anaongoza kwa kufuatiliwa sana na bado anaonekana mwenye mvuto zaidi.


NDUGU WA HARMORAPA KATIKA BIFU NA HARMONISE – CHAKA YES


Mwanamuziki wa Kizazi kipya anayechipukia kwa kasi anayefahamika kwa jina la Chaka Yes ambaye ni ndugu wa Harmorapa yuko tayari kuachia ngoma yake mpya aliyofanya katika studio za Combination Sound chini ya Producer Man Walter.
Akizungumza na MO Design, Mwanamuziki huyo aliyefahamika zamani kwa jina la Chaka Mlingula, amaesema kuwa Wimbo huo uitwao SALAM aliimba kwa kushirikiana na Producer huyo mwenye mbwembwe katika uimbaji Man Walter.

Kabla ya ngoma hiyo, Chaka Yes aliwahi kutamba na Ngoma inayokwenda kwa jina la Sidhani kama ntapendwa ambayo ilifanya vizuri katika vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii. Ngoma hiyo bado inaendelea kufanya vizuri ikiwa katika mfumo wa Audio na Video.

“ naachia kwanza ngoma hii ya Salam ikiwa ni audio tu, napenda mashabiki zangu waizowee kwanza ikiwemo na kunipamaoni na ushauri wao kabla sijafanya video” alisema Chaka,

“… unajua siku zote bila kupata maoni na ushauri wa watu wanaokufanya uendelee kuwa katika nafasi uliyopo, huwezi kufanya vizuri… so lazima nipate maoni ikiwemo na Baraka zao pia…” alimalizia chaka huku akicheka.

Chaka alisema ataanza maandalizi ya video baada ya kupata maoni kutoka kwa mashabi wake, kwani hapendi tena kufanya video itakayokuwa ya kawaida bali tu, anataka afanye video itakayowafanya mashabiki wa Harmonise wahamie kwake.



Alipoulizwa kwa nini anataka mashabiki wa Harmonise, akasema kuwa kiuwezo yeye ni zaidi ya Harmonise, kwanini msani huyo awe na mashabiki zaidi yake?.. So anataka kufanya kitu kitakachowaleta wale walioko kwa Harmonise warudi kwake kwani anaamini wote ni wa kwake lakini wako kule kwa vile walikuwa hawajamsikiliza vizuri yeye.

ALICHOKISEMA PROFESSOR JAY - BAADA YA DIAMOND KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA...

IKIWA ni saa chache baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kumkabidhi Bendera ya Taifa, msanii anayetikisa kwa wimbo wa Salome, Diamond Platnums, ambaye anaelekea nchini Gaboni kwa ajili ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa mashindano ya AFCON.
Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chadema na msanii mkongwe wa Hip Hop, Professor Jay amefurahishwa na kitendo hicho na kuamua kuonesha hisia zake wazi huku akimpongeza Diamond kwa hatua aliyofikia kwenye tasnia ya muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Professor Jay ameandika:

All the best SIMBAAA @diamondplatnumz  Bongo FLAVA inahitaji Wawakilishi wa kutoka TANZANIA wengi zaidi, UPENDO, UMOJA na MSHIKAMANO ndio silaha pekee itakayofanikisha hilo, Vinginevyo tutaendelea na kazi yetu ya siku zote ya KUPAKA RANGI UPEPO… #TeamTANZANIAKwanza  #AFCON

DIAMOND PLATNUMZ KUTUMBIZA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2017...

Staa wa Bongo Flava na Rais wa Wasafi,  Diamond Platnumz.
Staa wa Bongo Flava na Rais wa Wasafi,  Diamond Platnumz,  siku chache baada ya kutumbuiza kwa ustadi mkubwa kwenye tuzo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jijini Abuja nchini Nigeria, amealikwa  tena kutumbuiza kwenye ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 (AFCON 2017), Januari 14 nchini Gabon.
Staa huyo amewapa habari njema mashabiki wake kupitia mitandao ya Twitter na Instagram, kwa kupost taarifa ya shoo yake hiyo iliyowekwa kwenye akaunti maalum ya AFCON 2017.

“GABON!!! You know we gat to make a World History on the 14th January right?? See you this this Coming Weekend then… #WcbWasafi” aliandika.

NGOMA ZA TANZANIA ZAONGOZA KWA KUPENDWA KENYA 2016...

Video za muziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania ndizo zilizotazamwa zaidi na Wakenya katika mtandao wa YouTube, unaomilikiwa na Google, mwaka huu, takwimu zinaonyesha.
Video hizo zinatawala katika orodha ya video kumi zilizotazamwa zaidi, inayoongoza ikiwa video ya wimbo Salome, uliofanywa upya na Diamond Platnumz na Rayvanny.
Wimbo wa Work, wao Rihanna na Drake ni wa pili lakini kutoka hapo anaingia Diamond Platnumz na Harmonize wakiwa na wimbo wao Bado.
Video ya kwanza ya Wakenya kwenye orodha hiyo ni ya Sauti Sol kwa wimbo wao Unconditionally Bae, lakini bado kwenye wimbo huo walishirikiana na mwanamuziki Mtanzania, Alikiba.
Video nyingine za nyimbo katika orodha hiyo ni Work from Home wa Mmarekani Ty Dolla Sign na kundi la wasichana la Fifth Harmony, This is What You Came For wake raia wa Scotland Calvin Harris, Kwetu wake Rayvanny kutoka Tanzania, Cheap Thrills wao raia wa Australia Sia na Sean Paul wa Jamaica, Pillow Talk wa Mwingereza Zayn na Ain't Your Mama wa Mmarekani Jenniffer Lopez.
Orodha kamili:
  1. Salome - Diamond Platnumz na Rayvanny.
  2. Work - Rihanna na Drake
  3. Bado - Diamond Platnumz na Harmonize
  4. Sauti Sol - Unconditionally Bae, na Alikiba.
  5. Work from Home - Ty Dolla Sign na Fifth Harmony
  6. This is What You Came For - Calvin Harris
  7. Kwetu - Rayvanny
  8. Cheap Thrills - Sia na Sean Paul

WAKO HAPA WASHINDI WA TUZO ZA MTV AFRICA MUSIC AWARDS 2016



Mshindi wa tuzo ya Best Female Yemi Alade (Nigeria) akifanya mahojiano na MTV katika red Carpet ya MTV Africa Music Awards (MAMA) 2016 South Africa.

Yemi Alade (Nigeria) akiwa katika pozi.

Staa wa Bongo Fleva,  Diamond Platnumz (kulia) akiwa Yemi Alade.

Staa wa Nigeria Wizkid akipiga picha baadhi ya tuzo zake alizochukua usiku wa kuamkia leo.
Listi yote ya Washimdi

Best Live Act

Cassper Nyovest (South Africa)  – Winner
Eddy Kenzo (Uganda),
Flavour (Nigeria),
Mafikizolo (South Africa)
Stonebwoy (Ghana).

Best Group

Sauti Sol (Kenya)- Winner
Mi Casa (South Africa),
Navy Kenzo (Tanzania),
R2bees (Ghana)
Toofan (Togo).

Best Female

Yemi Alade (Nigeria) – Winner
Tiwa Savage (Nigeria)
Josey (Ivory Coast)
Mz Vee (Ghana)
Tiwa Savage (Nigeria)
Vanessa Mdee (Tanzania)

Best Pop/Alternative

Desmond & The Tutus (South Africa)
LCNVL (South Africa)
Shekinah (South Africa) / Kyle Deutsch (South Africa) – Winner
Timo ODV (South Africa)
Tresor (DRC)

Best International

Adele (UK)
Beyoncé (USA)
Drake (Canada) – Winner
Future (USA)
Rihanna (Barbados)

Best Lusophone Act

C4 Pedro (Angola) – Winner
NGA (Angola)
Lizha James (Mozambique)
Nelson Freitas (Netherlands/Cape Verde)
Preto Show (Angola)

Best Francophone Act

Franko (Cameroon)
J-Rio (Gabon)
Magasco (Cameroon)
Serge Beynaud (Ivory Coast) – Winner
Toofan (Togo)

Best Male

AKA (South Africa)
Black Coffee (South Africa)
Diamond (Tanzania)
Patoranking (Nigeria)
Wizkid (Nigeria) – Winner

Listener’s Choice

Adiouza (Senegal)
Bebe Cool (Uganda)
Burna Boy (Nigeria)
Den G (Liberia)
EL (Ghana)
Jah Prayzah (Zimbabwe) – Winner
Jay Rox (Zambia)
Kansoul (Kenya)
Kiss Daniel (Nigeria)
Lij Michael (Ethiopia)
LXG (Sierra Leone)
Meddy (Rwanda)
Messias Marioca (Mozambique)
Prince Kaybee (South Africa)
Reda Taliani (Algeria)
Saad Lamjarred (Morocco)
Sabri Mosbah (Tunisia)
Sidiki Diabate (Mali)
Tamer Hosny (Egypt)
The Dogg (Namibia)
Yamoto Band (Tanzania)

Best Collaboration in partnership with Absolut

AKA feat. Burna Boy, Khuli Chana & Yanga – “Baddest” (South Africa/Nigeria)
DJ Maphorisa feat. Wizkid & DJ Bucks – “Soweto Baby” ((South Africa/Nigeria) – Winner
Nasty C feat. Davido, Cassper – “Juice Back Remix” (Nigeria/South Africa) 
Patoranking feat. Sarkodie – “No Kissing” (Nigeria/Ghana) 
Sauti Sol feat. Alikiba – “Unconditionally Bae” (Kenya/Tanzania)

Video of the Year

“Jump” – Anatii & Cassper feat. Nasty C (South Africa); Director: Kyle Lewis
“Caviar Dreams” – AL Bairre & PhFAT (South Africa); Director: Daniel Levi
“If I Start to Talk” – Tiwa Savage feat. Dr Sid (Nigeria); Director: Clarence Peters
“Kisasi Kumi” – Sheeba (Uganda) – Director: Sasha Vybz
“ Niquer Ma Vie“ – Youssoupha (Congo) – Director: Antony Abdelli & Jose Eon – Winner

Personality of the Year in association with DStv

Caster Semenya (South Africa) – Winner
Linda Ikeji (Nigeria)
Pearl Thusi (South Africa)
Pierre Emerick Aubameyang (Gabon)
Wizkid (Nigeria)

Best Hip Hop in association with MTN

Emtee (South Africa) – Winner

Kiff No Beat (Ivory Coast)
Olamide (Nigeria)
Riky Rick (South Africa)  
Ycee (Nigeria)

Best Breakthrough

Babes Wodumo (South Africa)
Emtee (South Africa)
Falz (Nigeria)
Franko (Cameroon)
Nasty C (South Africa)
Nathi (South Africa)
Raymond (Tanzania)
Simi (Nigeria)
Tekno (Nigeria) – Winner

Song of the year in partnership with Google

“Shaktibobo” – Olamide (Nigeria)
“Reggae Blues” – Harrysongz feat Olamide, Kcee & Iyanya, Orezi (Nigeria)
“My Woman, My Everything” – Patoranking feat. Wande Coal (Nigeria) – Winner
“Godwin” – Korede Bello (Nigeria)
“Ngud” – Kwesta feat. Cassper (South Africa)
“Roll Up Re-Up” – Emtee feat. Wizkid and AKA (South Africa/Nigeria)
“Soweto Baby” – DJ Maphorisa feat. Wizkid (South Africa/Nigeria)
“Baddest” – AKA feat. Burna Boy, Khuli Chana, Yanga (South Africa/Nigeria)
“Wololo” – Babes Wodumo feat. Mampintsha (South Africa)
“Coller la Petite“ – Franko (Cameroon)
“Unconditionally bae” – Sauti Sol feat. Alikiba (Kenya/Tanzania)

Artist of the Year

Black Coffee (South Africa)
Diamond (Tanzania)
Sauti Sol (Kenya)
Wizkid (Nigeria)- Winner
Yemi Alade (Nigeria)

MAMA 2016 MTV Legend award goes to South African musician and human rights activist Hugh Masekela.

CHURA YA SNURA SASA KUONEKANA KWENYE TV NA RADIO...

Leo october 5 2016 Mrembo kutoka Bongo flevani Snura ambaye alizichukua
vichwa vya habari kadhaa baada ya wimbo wake wa Chura kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), leo kutoka kwa Snura, hatimaye wimbo wake umeruhisiwa kuchezwa kwenye Radio na Tv.
Snura amekutana leo na waandishi wa Habari na kuyasema mashariti ambayo ameyafata ili wimbo wake wa chura kupewa ruksa na Wizara... ‘Leo nimewaita hapa kwa sababu ya wimbo wangu wa chura kufunguliwa tena baada ya Serikali kuufungia tarehe  may 3 2016’>>>alisema Snura
‘Hii ni baada ya kukata rufaa na kukubaliana na Wizara kutengeneza Video nyingine ya wimbo wa Chura, "baada ya kutengeneza video mpya ndio wimbo wangu wa Chura umefunguliwa na ni ruksa kupigwa kwenye TV na Radio nchini, pia namshukuru sana Waziri Nape’>>>Snura

LIKO HAPA GAI JIPYA LA SAMATTA NA THAMANI YAKE

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji. Ameweka picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter na kuandika maneno ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, ‘Thanks God’.
xsamatta-jpg-pagespeed-ic-rtpxcedmupHili ndilo gari jipya la Mbwana Sammata.
Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.
Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo.
samatta…Muonekano wa nyuma wa gari hilo.
Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.
Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa League pamoja na ligi kuu nchini Ubelgiji japo amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha

UKO HAPA UTOFAUTI WA ALIKIBA NA DIAMOND KIMUZIKI...

KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiye anajua zaidi kuliko mwingine.
Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.
Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.
Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Alikiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.
Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.
Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.
Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.
Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.
Ambwene Yessaya ‘AY’ alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.
Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.
Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.
Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haoneshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.
Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.
Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa.
Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau.
© Copyright MO Design
Back To Top