
Filamu ya kwanza ya Kitanzania iliyochezwa katika maadhi halisi ya kitanzania itapatikana madukani hivi karibuni ikisambazwa na kampuni ya STEPS INTERTAINMENT ya Dar es Salaam Tanzania.
Akizungumza na MO Design kiongozi wa Kampuni hiyo Bwana Ravi, alisema kuwa filamu hiyo itakuja kuleta mapinduzi kwenye Tasnia hii kwani ni sinema ambayo imechezwa katika mahadhi halisi ya kitanzania "... mimi napenda tu kuwaambia watanzania wapenzi wa filamu wasikose kununua filamu ya IKINTU, kwani niu filamu nzuri sana iliyochezwa katika uhalisia wa Kitanzania, alafu ni picha isio na rugha za matusi wala mambo ya ajabuajabu, namaanisha ni filamu ambayo watu wanaweza kuingalia kifamilia..." alisema bwana Ravi.
Steringi katika filamu hii ni Mwanahabari, ambaye katika filamu hii ameigiza kwa kiwango kikubwa ambacho kimewashangaza mpaka wakongwe ambao walidhani kuwa Mwanahabari huyo hawezi kuigiza.
Filamu ya IKINTU imewakutasha wasanii wakongwe kama vile Kulwa Kikumba (Dude), Tafu Chuma, Mze Makatu ( Mze Chumo) Laeila Ernest (Jenifer), Miriam Robert, na Mussa Sikabwe (MO Design).
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.