Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

LIKO HAPA GAI JIPYA LA SAMATTA NA THAMANI YAKE

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji. Ameweka picha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter na kuandika maneno ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, ‘Thanks God’.
xsamatta-jpg-pagespeed-ic-rtpxcedmupHili ndilo gari jipya la Mbwana Sammata.
Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.
Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo.
samatta…Muonekano wa nyuma wa gari hilo.
Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.
Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa League pamoja na ligi kuu nchini Ubelgiji japo amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top