Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAHAKAMA YAKUBALI MAOMBI YA WADHAMINI CUF


Wakili wa wanachama wa Cuf, Juma Nassoro, akihojiwa na wanahabari baada ya kusikiliza shauri lao.

Baadhi ya wanachama wa Cuf wakiwa nje ya Mahakama Kuu.
Na Denis Mtima/Gpl
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetaja na kukubali maombi ya Bodi ya Baraza la Wadhamini la CUF dhidi ya Jaji Francis Mutungi ambapo yatasikilizwa wakati wowote wiki hii.
Katika maombi hayo namba 75 ya mwaka 2016 walalamikiwa wengine ni Prof. Ibrahim Lipumba na wanachama 12 wa chama hicho waliosimamishwa.
Bodi hiyo ya wadhamini ilifungua maombi hayo wiki iliyopita wakili wao akiwa ni Juma Nassoro wakiiomba mahakama itengue na kupitia uamuzi wa barua ya Jaji Mutungi kumtambua Lipumba kuwa mwenyekiti.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kutoka katika chumba cha kusikiliza shauri hilo, wakili Juma Nassoro amesema kuwa mahakama imekubali maombi hayo yaliyofunguliwa ya kuomba mahakama ifute barua ya msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, inayomtambua Lipumba kuwa mwenyekiti CUF.
Amesema pia mahakama imekubaliana na zuio lao la msajili kufanya kazi zake nje ya utaratibu ambao amepewa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top