Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

WALIOTUPA MADAWA YA KUTIBU BINADAMU UBUNGO, MBARONI....

ded-ubungo-7Mkurugenzi wa Mansipaa ya Ubungo, John L. Kayombo.ded-ubungo-1…Mkurugenzi akisisitiza jambo.ded-ubungo-6…Sehemu ya madawa hayo yaliyomwaga.
DAR ES SAALAM: Kampuni ya Indepth Scientific inayojihusisha na usambazaji wa madawa ya binadamu na vifaa tiba yenye makao yake mtaa wa Rose Mikocheni jijini Dar es Saalam, viongozi wake wametiwa mbaroni baada ya kubainika wametupa dawa za kutibu maradhi ya binadamu kwenye makazi ya watu.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo amesema:
“Mimi ni mkazi wa hapa Mpiji Majohe, Jumatano wiki iliyopita tuliona gari likimwaga takataka hapa, tukashtuka kwasababu siyo eneo la kutupa takataka, wakati bado wanamwaga tulifika na kuwazuia na tulipokagua tukaona ni madawa ya binadamu ya aina tofauti.
“Tulimpigia simu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo bwana , John L. Kayombo ambaye alifika eneo la tukio akiwa na askari na kuwahoji  dereva na mkuu wa msafara waliotambulika kwa majina ya Mzee Ali na Amosi ambao walijitetea kwa kusema wametumwa na meneja wao, Risper Monyangi.
“ Mkurugenzi akaamuru meneja huyo aje eneo la tukio, baada ya kufika na kubanwa na maswali alishindwa kujitetea na wote watatu walipelekwa kituo cha    Polisi cha Mbezi kwa Yusuph na kufunguliwa Mashtaka.”
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, John L. Kayombo  alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema:
“Ni kweli tukio limetokea na niwashukuru sana wakazi wa Mpiji Majohe kwa kunipa taarifa, nimesikitishwa sana na kitendo cha kampuni hii kumwaga madawa kwenye makazi ya watu kwa makusudi kabisa wameamua kuwaumiza raia wema na ili iwe mfano na fundisho ni lazima hatua kali zichuliwe dhidi yao.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda amesema:
“Bado tunaendelea na uchunguzi na watuhumiwa watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kujibu mashtaka yanayowakabili.”

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top