Tetemeko lingine baya la ardhi, limegonga maeneo ya katikati mwa Italia, mahali ambapo watu 300 waliuwawa mwezi Agosti mwaka huu.
Taarifa za awali zinasema kuwa uzito wa tetemeko hilo limefikia 6.6 katika vipimo vya Richa. Majumba kadhaa yameporomoka, likiwemo kanisa la St Benedict mjini Norcia. Hakuna taarifa zozote kuwahusu wahasiriwa au maafa. Kitovu cha tetemeko hilo lilikuwa kusini mashariki mwa mji wa Perushia. Uzito wa tetemeko hilo umesikika hadi mjini Roma, umbali wa kilomita 150.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.