Meneja wa Manchester City Pep Gurdiola anasema ushindi wa klabu hiyo wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona ni ushinidi mkubwa kwa klabu yake.
Manchester City hawajawai kuwashinda Barcelona kwenye mechi tano ambazo zimepita na Guardiola anasema kuwa ni jambo lili zuri kusema kuwa kwa mara ya kwanza wamecheza na klabu bora zaidi duniani na kuwashinda.
"Tumeshindana na Barcelona, lakini kwa sasa tumefanya kwa njia tofauti. Tulicheza mipira mirefu kwa sababu hatuko tayari kucheza jinsi wanavyocheza." alisema Guardiola.
Ushindi wa Man City unaweka katika nafasi ya pili kwenye jedwali nyuma ya Barcelona ikiwa sasa inahitaji ushindi mmoja zaidi kutoka kwa mechi mbili zilizosalia kuweza kusonga mbele kwa kundi la timu 16 bora.
Guardiola ambaye alishinda kombe mara mbili akiwa Meneja wa Barcelona, alipata kipigo wakati Man City ilishindwa kwa mabao 4-0 uwanja wa Nou Camp mwezi uliopita.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.