Kiungo wa kati wa Manchester City amesalimu amri na kumuomba msamaha wasimamizi wa klabu hiyo baada ya kutochezeshwa kwa muda na meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola.
Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema: "Naomba radhi - kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha - wasimamizi wa timu na wote wanaofanya kazi katika klabu hii kwa sababu ya sitafahamu zilizotokea awali.
"Matamshi hayo hayawakilishi msimamo wangu kuhusu klabu au watu wanaofanya kazi katika klabu hii."
Toure mwenye umri wa miaka 33 ameichezea City mara moja msimu huu na aliwachwa nje katika kikosi cha vilabu bingwa Ulaya.
Ajenti wake Dimitri Seluk amesema kuwa kiungo huyo wa kati ''alifedheheshwa'' na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang'anyiro hicho.
Guardiola:''lazima aombe msamaha la sivyo hatocheza''.
Raia huyo wa Uhispania pia anataka msamaha kutoka kwa Seluk.
Alisema kuwa ni uamuzi mgumu kumwacha nje Toure katika kikosi cha kombe la Vilabu bingwa Ulaya.
''Iwapo ana tatizo anafaa kuzungumza wenzake katika klabu ,alisema Gurdiola,ambaye alikuwa mkufunzi wa Barcelona wakati Toure alipouzwa kwa Manchester City 2010.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.