Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KANISA LA WATU WEUSI LACHOMWA MOTO MAREKANI...

Polisi katika jimbo la Marekani la Mississippi wanasema wanachunguza uhalifu wa chuki baada ya Kanisa linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa na kisha kuchorwa maneno ya kusema: "Mpigie kura Trump".
Kanisa hilo linalopatikana eneo la Greenville lilijengwa miaka 111 iliyopita. Msimamizi wa kituo cha zima Moto alisema kuwa moto katika Kanisa la Hopewell Missionary Baptist Church uliwashwa makusudi.
Shambulio hilo limetokea wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Jumanne wiki ijayo. Maafisa wanasema ujumbe ulioandikwa kwenye jumba hilo ni wa kuzua hofu. Meya wa Greenville, Mississippi amesema kisa hitendo hicho ni cha 
"chuki na woga" na s"shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa watu kuabudu".
Kisa hicho kinawakumbusha watu kuhusu visa vya kuchomwa moto kwa makanisa ya watu weusi miaka ya 1950 na 1960, watu weusi waliokuwa wanapigania haki zao.
Maafisa wa FBI wakishirikiana na wachunguzi wa jinai wa jimbo la Mississippi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top