Mwimbaji wa nyimbo za injili Haika Mtokoma ametambulisha rasmi na kwa mara ya kwanza kabisa Video ya Wimbo wake INALIPA KWA YESU NDANI YA MO Design Tv.
Akiongea na Mwandishi wetu Haika amesema Kuwa Wimbo huo ni mmoja kati ya njyimbo saba zitakazokuwa ndani ya album yake inayokwenda kwa jina la NIKO BIZE NA YESU, amesema kuwa ameanza kwa kutambulisha wimbo huo kwanza kwa vile bado yupo kwenye ukamilishaji wa video za nyimbo zilizosalia ikiwemo ule unaobeba jina la album
amesema kuwa video zote zinafanyika na Kampuni ya MO Design chini ya Director MO akiwa ndiye pia aliye andaa audio ya nyimbo hizo.
Haika amesema anaomba Watanzania na wote watakaoitazama video hii wamuunge mkono kwa maombi kwani safari yake bado mbichi katika kumuimbia Mungu. lakini pia alihitimisha kwa kusema kuwa yuko tayari kwa mialiko ya aina yoyote ile ambayo ni ya kumtukuza Mungu.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.