Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KIONGOZI WA UPINZANI ASHINDA URAIS GHANA...

Mwanasiasa mkongwe ameshinda uchaguzi wa urais nchini Ghana, ushindi ambao umepokelewa kwa shangwe na nderemo na wafuasi wake.
Nana Akufo-Addo, alishangilia ushindi wake na kusema taifa hilo sasa ni mwenge wa demokrasia Afrika Magharibi.
Ameahidi kukabiliana na uchumi uliozorota, swala ambalo lilitiliwa mkazo wakati wote wa kampeni,
Bw Akufo-Addo alisema kuwa ushindi wake ni hatua anayofurahia sana katika maisha yake yote na akaahidi kuwa atafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa anatekeleza matakwa ya wananchi wa Ghana.
Amepongezwa na mshindani wake mkuu, rais John Mahama, aliyeahidi kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top