Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

UTATA KUHUSU HATMA YA FARU AITWAYE JOHN TANZANIA

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka maafisa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kutoa ufafanuzi kuhusu kuhamishwa kwa faru maarufu kwa jina la John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
Bw Majaliwa amewataka viongozi wa NCAA kuwasilisha kwake nyaraka zote zilizotumika katika kumuhamisha faru huyo kufikia Alhamisi.
Alisema ana taarifa kuwa faru huyo John alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti katika eneo la Serengeti mnamo 17 Desemba, 2015.
"… mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200 ambapo mkapewa shilingimilioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100 nyingine baadaye," alisema Bw Majaliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania, Bw Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa zozote kumhusu faru huyo ambazo zimetolewa.
"Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,".
Bw Majaliwa pia alimsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili.
Kwa sasa, anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haiwezekani mtumishi awe anachunguzwa na Takukuru halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini," alisema.
Hifadhi ya Ngorongoro ndilo eneo pekee Tanzania ambapo faru wanapatikana kwa wingi porini, ndani ya kreta.
Inakadiriwa kwamba idadi ya faru katika hifadhi hiyo ni takriban 35

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top