Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

VIDEO... SAFARI YA FRANCIS CHEKA NCHINI INDIA



Mwanamasumbwi Champion wa Tanzania na ambaye anashikilia mkanda wa uzito wa juu Francis Cheka, ameanza safari yake kuelekea nchini India katika mji wa New Delly kwa Ajili ya mpambano dhidi yake na mpambanaji wa kihindi ajulikanae kwa jina la Vigender Sigh.

Akiongea na MO Design Tv katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Cheka alisema kuwa safari yake ni ya kwenda kuchukua ushindi wake na kurejea nao Tanzania kwani Vigender hana uwezo wa kupambana naye.

Fancis aliondoka uwanja wa ndege akiwa ameongozana na Promoter wake ambaye ni Juma Msangi a.k.a J. Msangi.
Lakini pia, imekuwa ni safari ya kwanza ya Francis Cheka kusafiri kwenda kwenye mapambano ya nje ya nchi akiwa ameongozana na Kocha wake Abdallah Komando.

Promoter J. Msangi alisema kuwa anayo imani na francis na kuwa anaamini kuwa Francis anakwenda kufanya vizuri kwani mazoezi aliyofanya yanampa imani kubwa.
lakini pia kwa upande wake Kocha Abdallah Komando alisema kuwa siku zote yeye anamuamini Francis hasa pale anapokuwa amefanya mazoezi ya kuridhisha, hivyo anaamini kuwa francis anakwenda kuleta ushindi.

VIDEO HII HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top