Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MWANZILISHI WA JAMII FORUMS MIKONONI MWA POLISI

Mwanzilishi wa mtandao maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wa Jamii Forums Maxence Melo anashikiliwa na polisi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jamii Forums Melo anashikiliwa kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo wa Jamii Forums.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatano asubuhi.
Akizungumza na Mwandishi wa BBC Swahili Sammy Awami, mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Mike Mushi naye alisema kuwa kukamatwa kwa Maxence Melo ni utekelezwaji wa sheria ya makosa ya mtandaoni kwa sababu wanaosimamia kesi hii ni watu wa kitengo cha cyber crimes yaani kitengo cha makosa ya kimtandao katika jeshi la polisi.
Akijibu swali la Sammy, Mike mushi amesema kuwa sheria hii ni kandamizi kwa uhuru wa habari nchini.
Source: BBC Swahili

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top