Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ALIYEKUWA RAIS WA GAMBIA KUACHIA MADARAKA... AWASILI EQUATORIAL GUINEA

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili nchini Equatorial Guinea, siku moja baada ya kuachia madaraka kwa Adama Barrow, aliyemshinda katika uchaguzi wa urais mwezi Disemba mwaka jana.
Jammeh alisafiri kwa ndege kutoka Banjul hadi Guinea na baadaye kuendelea na safari yake kwenda Equatorial Guinea.
Hapo jana Bwana Jammeh alitangaza kwamba atang'atuka baada kuongoza Gambia kwa miaka 22.
Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili nchini Guinea . Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake nchini Gambia kumshurutisha Bwana Jammeh kukubali Adama Barrow aapishwe.
Jumuiya hiyo inasema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watasalia nchini humo kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top