Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

TRUMP AVISHAMBULIA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUAPISHWA KWAKE...

Siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua hatamu y a uongozi wa taifa hilo, amelaamu baadhi ya vyombo vya habari kwa kueneza taarifa za uongo juu ya idadi ya watu waliyohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.
Trump amesema zaidi ya watu milioni moja walihuthuria shere hiyo.
Msemaji wa White House, Sean Spicer,amesema vyombo hivyo vya habari vinaendesha kampeni ya kugawanya watu kwa kuangazia habari ambazo hazina msingi wowote.
Hata hivyo kanda za video za matangazo ya moja kwa moja wakati wa hafla hiyo hazikunasa umati mkubwa wa watu.
Picha zinaonekana zikionyesha watu wengi waliohudhuria shereha ya kupiashwa kwa rais Barack Obama mwaka 2009.
Bwana Trumpo hakuzungumzia maandamano wakati alitembelea makao makuu ya CIA jimbo la Virginia siku ya Jumamosi, lakini badala yake alishambulia vyombo vya habari.
Bwana Trump alisema kuwa video na picha wakati wa kuapishwa kwake zilionyesha taarifa ziziso za ukweli.
"Walionekana kama watu milioni 1.5 siku nya Ijumaa, alisema Trump, na kuzua ripoti za vyombo vya habari kuwa walikuwa wati chini ya 250,000.
Rais huyo mpya aliwataja waandishi wa habari kuwa watu waongo zaidi duniani.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top