Mwana anga wa Marekani Gene Cernan, aliyekuwa binadamu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, amefariki dunia akiwa na miaka 82.
Shirika la anga za juu la Marekani Nasa limesema limehuzunishwa sana kumpoteza mwana anga huyo mstaafu.
Cernan alikuwa mmoja wa watu watatu pekee waliowahi kwenda Mwezini mara tatu na ndiye binadamu aliyeukanyaga Mwezi mara ya mwisho kabisa, mwaka 1972.
Maneno yake ya mwisho aliyoyasema kabla ya kuondoka kwenye Mwezi yalikuwa: "Tunaondoka jinsi tulivyokuja na, Mungu akitujalia, tutarejea na amani na matumaini kwa binadamu wote."
Alikuwa kamanda wa chombo cha anga za juu cha Apollo 17 wakati huo.
Ni watu 12 pekee waliowahi kutembea kwenye Mwezi, na kati yao ni sita pekee ambao bado wako hai.
Kupitia taarifa, familia ya Cernan imesema alifariki dunia Jumatatu baada ya kupata matatizo ya kiafya.
Hawakutoa maelezo zaidi.
Kabla ya kufanya safari ya Apollo 17, Cernan alikuwa amesafiri anga za juu mara mbili awali - mwaka 1966 na 1969.
Alistaafy mwaka 1976 na akaingilia biashara kibinafsi. Alikuwa mara kwa mara akichangia katika runinga kuhusu masuala mbalimbali.
Cernan pia aliandaa makala ya video kuhusu maisha yake.
Alizaliwa 14 Machi 1934 mjini Chicago, na jina lake kamili ni Eugene Andrew Cernan.
Ameacha mjane Jan Nanna Cernan, bintiye na binti wawili wa kambo pamoja na wajukuu wanane.
Kifo chake kilitokea wiki chache baada ya mwana anga mwingine wa Nasa John Glenn kufariki dunia.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.