IKIWA ni saa chache baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kumkabidhi Bendera ya Taifa, msanii anayetikisa kwa wimbo wa Salome, Diamond Platnums, ambaye anaelekea nchini Gaboni kwa ajili ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa mashindano ya AFCON.
Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chadema na msanii mkongwe wa Hip Hop, Professor Jay amefurahishwa na kitendo hicho na kuamua kuonesha hisia zake wazi huku akimpongeza Diamond kwa hatua aliyofikia kwenye tasnia ya muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Professor Jay ameandika:
All the best SIMBAAA @diamondplatnumz Bongo FLAVA inahitaji Wawakilishi wa kutoka TANZANIA wengi zaidi, UPENDO, UMOJA na MSHIKAMANO ndio silaha pekee itakayofanikisha hilo, Vinginevyo tutaendelea na kazi yetu ya siku zote ya KUPAKA RANGI UPEPO… #TeamTANZANIAKwanza #AFCON
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.