Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ALICHOKISEMA MBWANA SAMATTA, MECHI YA LEO DHIDI YA BOTSWANA...

KIKOSI cha Taifa Stars, kikiongozwa na nahodha Mbwana Samatta leo kinacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Botswana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kimeahidi ushindi.
Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji iliyofuzu kucheza robo fainali ya Europa League, amesema pamoja na wachezaji wenzake watapambana kuhakikisha wanaifunga Botswana leo.
“Mimi na wachezaji wenzangu wote kwa pamoja tunatakiwa kuwaonyesha Watanzania kwamba hii mechi ni muhimu kwetu, hivyo tutapambana kuleta ushindi na itakuwa vizuri kwani tupo nyumbani,”alisema Samatta.
Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, yeye alisema: “Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, ukiangalia vikosi vyote vina chipukizi wengi, hivyo tunatarajia mechi itakuwa nzuri kwa pande zote.
“Hii ndiyo mechi yangu ya kwanza nikiwa kocha mkuu, nimejipanga kufanya vizuri kwa sababu si mgeni na timu hii kutokana na kwamba huko nyuma nilikuwa kocha msaidizi.”
Wakati huohuo, Kocha wa Botswana, Peter Buffler, alisema: “Japo siwajui wachezaji wa Tanzania (Taifa Stars), lakini tumekuja kupambana nao kusaka ushindi, licha ya kuwa mchezo wenyewe ni wa kirafiki, ni muhimu kushinda na tunaamini tutafanya vizuri.”

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top