Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

NDUGU WA HARMORAPA KATIKA BIFU NA HARMONISE – CHAKA YES


Mwanamuziki wa Kizazi kipya anayechipukia kwa kasi anayefahamika kwa jina la Chaka Yes ambaye ni ndugu wa Harmorapa yuko tayari kuachia ngoma yake mpya aliyofanya katika studio za Combination Sound chini ya Producer Man Walter.
Akizungumza na MO Design, Mwanamuziki huyo aliyefahamika zamani kwa jina la Chaka Mlingula, amaesema kuwa Wimbo huo uitwao SALAM aliimba kwa kushirikiana na Producer huyo mwenye mbwembwe katika uimbaji Man Walter.

Kabla ya ngoma hiyo, Chaka Yes aliwahi kutamba na Ngoma inayokwenda kwa jina la Sidhani kama ntapendwa ambayo ilifanya vizuri katika vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii. Ngoma hiyo bado inaendelea kufanya vizuri ikiwa katika mfumo wa Audio na Video.

“ naachia kwanza ngoma hii ya Salam ikiwa ni audio tu, napenda mashabiki zangu waizowee kwanza ikiwemo na kunipamaoni na ushauri wao kabla sijafanya video” alisema Chaka,

“… unajua siku zote bila kupata maoni na ushauri wa watu wanaokufanya uendelee kuwa katika nafasi uliyopo, huwezi kufanya vizuri… so lazima nipate maoni ikiwemo na Baraka zao pia…” alimalizia chaka huku akicheka.

Chaka alisema ataanza maandalizi ya video baada ya kupata maoni kutoka kwa mashabi wake, kwani hapendi tena kufanya video itakayokuwa ya kawaida bali tu, anataka afanye video itakayowafanya mashabiki wa Harmonise wahamie kwake.



Alipoulizwa kwa nini anataka mashabiki wa Harmonise, akasema kuwa kiuwezo yeye ni zaidi ya Harmonise, kwanini msani huyo awe na mashabiki zaidi yake?.. So anataka kufanya kitu kitakachowaleta wale walioko kwa Harmonise warudi kwake kwani anaamini wote ni wa kwake lakini wako kule kwa vile walikuwa hawajamsikiliza vizuri yeye.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top