Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

UPELELEZI KESI YA WEMA SEPETU WAMSHANGAZA HAKIMU...



JANA Aprili 12, nyota wa sinema za Bongo, Wema Sepetu alipanda tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar kusikiliza kesi ya tuhuma za kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya ambapo upande wa jamhuri umeshindwa kukamilisha upelelezi dhidi ya kesi inayomkabili msanii huyo.



Upande wa mashtaka uliowakilishwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula ulisema kesi hiyo ilifika kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika hivyo akaomba ipangiwe tarehe nyingine.
Ndipo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipohoji iweje upande wa jamhuri icheleweshe upelelezi wa kesi hiyo ambapo kila tarehe inayotajwa serikali inadai upelelezi haujakamilika, akaiharisha kesi hiyo mpaka Mei 2, mwaka huu.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top