Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

HAYA HAPA MAMBO 18 CHADEMA IMEZUNGUZIA NA WANAHABARI LEO DAR...



Leo July 31, 2017 Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA kupitia Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe imekutana na Waandishia wa Habari katika mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, CHADEMA imetoa taarifa ya maazimio baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho kukutana kwa siku mbili mfululizo July 29-30, 2017 katika Hotel ya Double Tree, Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zao
1.".. Serikali ituambie ina mpango gani wa muda mfupi kuokoa hali yetu ya kiuchumi.. " -          Mbowe
2. "... Hatuchukii mapambano ya kutafuta haki kwenye rasilimali zetu lakini ufanyike utafiti         wa kutosha... " - Mbowe
3.  "...Kwa sababu tumeshindwa kuzalisha ndani, Serikali inakopa sana nje bila kujua nani        atalipa... " - Mbowe
4. "... Kitu pekee ambacho kimeongezeka kwa kuingizwa nchini ni chakula..." - Mbowe
5. "... Takwimu za benki kuu zinasema kuwa kwenye benki za biashara Viwanda vimekopa       0%" - Mbowe
6. "... Viwanda vingi vimefungwa kwa sababu ya kodi mbaya hazilipiki, gharama ya kufanya     biashara TZ ni maumivu makubwa sana... " - Mbowe
7. ".. Viwanda vingi vilishindwa kuendeshwa kwa sababu vingi vilikuwa na teknolojia ya             zamani"-Mbowe
8. "... Viwanda ambavyo vilibinafsishwa vilikuwa vinaendeshwa kwa hasara... " - Mbowe
9. "... Viwanda vingi vilifungwa kwa sababu vilishindwa kujiendesha..." - Mbowe
10. "... Hakuna mfanyabiashara duniani ambaye atapewa kitega uchumi ambacho                       kinamuongezea faida akaamua kukifunga sababu anaichukia TZ..." - Mbowe
11. "Si kweli kuwa kila mfanyabiashara ni mpiga dili... " - Mbowe
12. "... Tutaambiwa uchumi unakua lakini umasikini unaongezeka, uchumi unakua mifukoni         mwa wale walioko kwenye sekta ambazo zinakua sio kilimo... " - Mbowe
13."... Wakati nchi nyingine zinasaidia wananchi kuzalisha vyakula lakini Serikali yetu                 inapunguza..." - Mbowe
14. "... Mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii miwili vitu vimepanda bei lakini kipato cha wananchi hakijaongezeka... " - Mbowe
15. "...Usalama wa taifa ni usalama wa chakula, kama hakuna usalama wa chakula hakuna       usalama wa Taifa..." - Mbowe
16. "... Wafanyabiashara wanapolia uchumi unaporomoka, ni kweli unaporomoka... " -                 Mbowe
17. "... Leo tutatumia taarifa za benki kuu, hatuna mashaka kwa kuwa taarifa za benki kuu          ndio taarifa za Serikali... " - Mbowe
18. "... Leo tutazungumzia kuhusiana na hali ya uchumi wa nchi yetu... " - Mbowe

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top