Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KUPIMA UKIMWI NI LAZIMA - ZAMBIA

Rais wa Zambia Edga Lungu amesema kuwa kwa sasa ni lazima kila mtu apimwe hali yake ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo.
Zambia ni kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya ukimwi kusini mwa bara la Afrika kwa asilimia 11.6, huku watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wakiwa na wanaishi na virusi vya ukimwi
Bwana Lungu alisema kuwa kupimwa na kupewa ushauri na matibabu sio kitu cha kujitolea, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchimi humo.
Alitoa tangazo hilo wakati wa uzinduzi wa baraza la ukimwi  mji mkuu wa Zambia - Lusaka.
Bwana Lungu alisema kuwa suala hilo limezungumziwa na baraza la mawaziri.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top