Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), leo amefunguka juu ya suala la ulinzi na usalama wa wananchi wa Tanzania na kueleza jinsi alivyosikitishwa na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na kuunga mkono kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba, kwa sasa nchi yetu haipo katika hali ya usalama na pia ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Kamati ya Usalama na Ulinzi ya Bunge kutowasilisha ripoti ya kushambuliwa kwa Mbunge Lissu kwa sababu zisizokuwa na mashiko na kuwanyima wabunge kuchangia mawazo yao juu ya usalama wao na watu wao.
Hata Hivyo, Spika Ndugai alisema kuwa, kushindwa kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kulitokana na kamati hiyo kutoikamilisha hivyo wataiwasilisha kwenye kikao kijacho cha bunge.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.