Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

TIKETI KOMBE LA DUNIA 2018 ZAANZA KUUZWA RUSSIA...

Kundi la kwanza la tiketi za fainali za Kombe la Dunia 2018 ambazo zitachezewa nchini Urusi zilianza kuuzwa Alhamisi.
Mashabiki wa soka wanaweza kuwasilisha maombi ya kununua tiketi hizo kupitia tovuti ya Fifa.
Tiketi hizo zitauzwa kwa awamu mbili.
Bei ya tiketi hizo itakuwa ni kuanzia £79 kwa mechi za raundi ya pili hatua ya makundi hadi £829 kwa fainali yenyewe ambayo itachezewa Moscow.
Kwa kufuata sera za awali za uuzaji wa tiketi, wakazi wa urusi watakuwa na aina maalum za tiketi ambazo bei yake itaanzia £17.
Tiketi ghali zaidi zitakuwa za mechi ya fainali yenyewe ambazo zitauzwa £829.
Hilo litakuwa ni ongezeko la £151 ukilinganisha na tiketi za mechi sawa za fainali ya mwaka 2014 ambayo ilichezewa Rio de Janeiro nchini Brazil.
"Tumeweka mfumo wa kutoa tiketi ambao utawapa mashabiki nafasi sawa ya kujipatia tiketi," katibu mkuu wa Fifa Fatma Samoura amesema.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top