Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KWA HERI MR. NICE

Anaitwa LUCAS MKENDA, kwa jina la ugali kama wasemavyo wa janja au jina maarufu ni MR. NICE... nikinara wa mziki wa takeu aliyeshika vilivyo katika kipindi chake. Alikuwa hana mpinzani na ni msanii ambaye alikuwa anaongoza sokoni kwa mauzo kuliko msanii mwingine yeyote.
Mr. NICE alishika sana katika miondoko ya takeu mpaka akafikia kuitwa mfalme wa takeu. Style ambayo alibuniwa na Producer wake ajulikaye kwa jina la KAMETA. Hakika ni KAMETA ndio aliyemtoa Mr. NICE na kumfikisha katika nafasi ile aliyokuwa akiishikilia.
Aling'ara sana kwa nyimbo zake kama FAGILIA BONGO, KUKU KAPANDA BASKELI na nyingine nyingi, nyimbo ambazo zilipendwa sana na watu wote hasa watoto. Mr. NICE alipata mafanikio makubwa kupitia mauzo ya kazi zake, lakini haikujulikana pesa alikuwa akizipeleka wapi, maana inasemekana alikuwa mtu wakupenda sana starehe kama walivyo baadhi ya wasanii wengine wa bongo. Mr. NCE akiingia baa basi wote watakao kaajirani na meza yeke wataneemeka kwa ofa.


Lakini sasa ni kama imebaki historia, Mr. NICE kwisha kazi, amejitahidi kutaka kurudi lakini imeshindikana haijulikani ni nini, wengine wanasema ni laana ya Producer wake KAMETA. mafanikio yalipozidi na kujiona kwamba anaweza sana Mr. NICE alimkana na kuamua kuachana na Producer wake ambaye ndiye aliyemfikisha alikokuwa amefikia, na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba aliachana naye kwa kashfa huku akimponda kuwa ma producer sio peke yake, na ambapo KAMETA akajibu kuwa akiachana na yeye itakuwa ndio mwisho wake. sio kwamba amerogwa hapana ila inasemekana kuwa hakuna producer mwengine ambaye angeweza kumpatia Mr. NICE zaidi ya KAMETA.
Unajua waswahili wanasema kila shetani na mbuyu wake, nice aliuchezea mbuyu wake akaukataa sasa amepotea Kwa taarifa zilizopatikana hivi karibuni na zilizoandikwa na moja ya magazeti yanayotoka mara mbili kwa wiki, ni kwamba Mr. NICE amerudi kijijini kabisa baada ya kuona maisha yazidi kuwa magumu.
Inasemekana alionekana akiwa anapakia vitu vyake kwenye gari lake kwa ajili ya kuondoka kijijini kwao. Hii inasikitisha na inabidi wasanii wengine wajifunze kupitia kwa Mr. nice ili waweze kuendelea vizuri na kazi yao ambayo waliichagua kuifanya ambayo ni sanaa... Starehe ni nzuri lakini mwisho siku zote huwa sio mzuri...

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top