ILIPOISHIA SEHEMU YA 12
... Muda ulikuwa umekwenda sana, ilikuwa tayari ni saa saba na dakika ishirini na sita. Hasina alikuwa akiingia nyumbani huku akiwa amebeba kapu la vyakula walivyonunuwa asubuhi na Bi. Pauline mke wa mzee Bisu na huku mkono mwingine akiwa amebeba begi lililosheheni nguo alizonunuliwa na mzee Bisu. mpaka muda huo alikuwa hajaanda chochote kwa ajili ya chakula cha mchana...
SASA ENDELEA NA SEHEMU YA 13
... Mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio, aliamini kabisa kuwa Bi. Pauline alikuwa tayari karudi na alikuwa akijiuliza cha kumuambia pale atakapoulizwa alikokuwa muda wote ule toka walivyoachana kule sokoni. amwambie kuwa baba alimuambia waende guesti, weee!!! kama hajitaki asubutu kusema hivyo aone balaa lake.
alizidi kuusogelea mlango wa kuingilia ndani huku kichwani akiwa hajajua atasema nini pale atakapoulizwa alikokuwa. mapigo yalizidi kumuenda mbio pale alipokishika kitasa na kutaka kukizenguusha ili kuufungua mlango, lakini ghafla aliona kitasa hicho kikizunguuka na mara mlango ukafunguliwa, ilikuwa kidogo atoke mbio kwani alijuwa ndo tayari anakabiliana ana kwa ana na Bi. Pauline. lakini ghafla moyo wake ulitulia pale alipomuona aliyefungua mlango huo kuwa sio aliyemtegemea, alikuwa ni Denis mtoto wa mwisho wa mzee Bisu.
"... we dada unatoka wapi saa hizi..."
Denis alimuhoji mara tu baada ya kumuona pale mlangoni.
"... natoka sokoni..."
alijibu Hasina huku akiwa anaingia ndani baada ya denis kumpisha
"... sokoni ndo mpaka saa hizi?.. sasa utapika saa ngapi na watu tule saa ngapi..."
"... sasa hivi tu naanza kupika na chakula kitakuwa tayari ndani ya muda mfupi..." alijibu tena Hasina huku akielekea jikoni ambako aliliacha lile kapu lenye chakula kisha akachukuwa begi lake lenye nguo akaingia nalo chumbani kwake.
Denis alikuwa akimuangalia tu bila kuongeza neno,. alikuwa akitamani kumuuliza maswali mengi kulingana na kuchelewa kwake kutoka sokoni pia na kuhusiana na lile begi lakini aliamua tu kukaa kimya. alitoka zake nje na kuondoka kwenda kwenye mambo yake mengine.
huku ndani Hasina hakupenda kupoteza muda, aliingia jikoni na kuanza kukorofisha harakaharaka, aliangalia chakula ambacho anaweza kukiandaa na kikawa tayari ndani ya muda mfupi ili watu au Bi. pauline asije akaleta utata.
hata hivyo pamoja na kuwa muda ulikuwa umekwenda sana hakuna mtu aliyewahi kurudi nyumbani siku hiyo, hata Denis alivyoondoka ilikuwa kimoja, hakurudi tena kwa ajili ya chakula. bahati ilikuwa upande wake kwani mtu wa kwanza kurudi nyumbani siku hiyo alikuwa Bi. pauline na ilikuwa tayari ni saa kumi jioni, Hasina alikuwa tayari keshapika chakula na kukihifadhi vizuri, hivyo Bi. pauline alipoingia, hakuwa na maswali zaidi ya kumwambia hasina ampe chakula kwani njaa inamuuma.
bila kuchelewa Hasina alimuandalia chakula nakumtengea vizuri kisha yeye akarudi zake jikoni kuendelea na mambo mengine.
pamoja na kuwa tayari alikuwa ameokoka katika tatizo la kuchelewa kurudi nyumbani, lakini bado moyoni mwake alikuwa na hofu, alikuwa akijihisi kukosa amani kila alipokutana na Bi. pauline. kwani kila alipofikiria kile alichokifanya na mzee Bisu, alijikuta akimuogopa Bi. pauline. kitendo hicho kilimfanya akae jikoni muda wote bila hata kutoka kama inavyokuwa kawaida yake mara atoke aingie huku na kule, alikuwa akiogopa kukutanisha macho yake na ya Bi. pauline aliyekuwa amekaa muda wote pale sebuleni akiangalia tv.
saa kumi na moja na nusu mzee Bisu aliingia akasalimiana na mkewe kisha akaingia chumbani ambako alibadilisha nguo na kuja kukaa sebuleni na mkewe.
"... mmeshindaje hapa leo?.. alihoji mara baada ya kukaa kwenye sofa lililokuwa jirani na lile alilokalia mkewe huku wote wakiwa wameelekea kwenye tv.
"... tumeshinda salama tu.."
"... vipi wanao wote hawajarudi?.." aliendelea na maswali huku akiangaza angaza huku na huku kama atafanikiwa kumuona Hasina lakini hakuambulia kitu.
"...hawajarudi hata mmoja na wala hata chakula cha mchana hapa hakijaliwa..."
mzee bisu alishituka kusikia chakula cha mchana Hakijaliwa, katika akili yake akajua kuwa labda hali hiyo ilijitokeza kulingana na kuchelewa kwa Hasina. akajua hapa soo, Hasina kama atakuwa amehojiwa maswali anaweza akawa ameropoka. akajaribu kumuangali machoni mke wake aone kama kuna kitu kitamfanya agundue kitu chochote cha hatari lakini haikuwa hivyo, akatuliza kwanza akili yake na kuhoji.
"... unasema chakula cha mchana hakijaliwa?.. tatizo ni nini?.."
"... tatizo si wanao wenyewe hawajarudi, kwa hiyo chakula kimepikwa hakijapata mlaji..."
mzee Bisu akashusha pumzi ndefu japo kimyakimya, kisha akajiweka sawa pale kwenye sofa.
"...na Hasina yukom wapi?.."
"... yuko jikoni huko, na leo naona kajijimbia huko jikoni hataki kutoka..."
"... hem niitie aniletee maji ya kunywa..."
ukweli sio kama alikuwa akihitaji maji ila alitaka tu amuone Hasina amlinganishe tena na kile alichomfanyia muda mfupi uliopita. mpaka sasa alikuwa bado anashindwa kumpatia picha Hasina kulingana na udogo wake na mambo yake ya falagha yalivyokuwa makubwa.
"... Hasinaaa!!!" aliita Bi. Pauline.
"... Beee..." sauti ya Hasina ilisikika kutoka jikoni.
ITAENDELEA......
USIKOSE SEHEMU YA 14
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN