Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

BABU JADI AMEKUJA KWAAJILI YA AKINA DIAMOND

BABU JADI AKITUMBWIZA NJE YA JENGO LA STUDIO ZA ECK PRODUCTION
PEMBENI YAKE NI "G " WA DODOMA
Babu Jadi, ni mwana muziki wa nyimbo au muziki wa asili kutoka Dodoma.
aliwasili jiji Dar es Salaam kwa ajili ya kurekodi album yake ya nyimbo hizo za asili.
Aliibukia katika studio za Eck Production Magomeni Mwembechai ambako ndiko anakofanyia kazi yake hiyo ya album ya nyimbo za asili.
BABU JADI AKIONESHA JINSI YA KUCHEZA MUZIKI WA JADI HUKU AKITUMBWIZA
akiongea na Modesign Babu Jadi alisema kuwa amekuja kuwaonesha watanzania kuwa muziki wanaofanya hawa watoto akina Diamond sio muziki ila muziki wa kweli ni huo anaoufanya yeye.

Babu Jadi alisema kuwa hata ukichunguza vyombo vya muziki vinavyotumika kutengenezea muziki wa akina Diamond vyote vinapitia katika tyuni za vyombo vya Jadi.
Babu jadi amesema kuwa Album yake itakuwa na jumla ya nyimbo tisa na itasambazwa na kampuni ya GMC
"... sasa hivi niko kwenye Hatua za mwisho na hivi karibuni itakuwa tayari... nataka kuwaonesha watanzania kuwa vijana wanadanganyika na muziki huu wa akina Diamond sasa wasubiri kusikia muziki wa kweli.." alisema babu Jadi.

Producer anayesimamia album ya Babu Jadi ni yule yule aliyetengeneza album ya UTAMU WA YESU ya Rose Muhando na DUNIA HAINA HURUMA ya Bahati Bukuku anayejulikana kwa jina la Enock Nyongoto au Producer Eck. hivyo tutarajie kitu kikubwa sana kutoka kwa Babu Jadi


BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top