... mzee Bisu hakupenda kupoteza muda, alichomoka kama mshale na kwenda kusimama katikati ya sebule. wakati anafunga breki tu akakutanisha macho na mwanaye Dennis ambaye naye alikuwa ndo anaingia kutokea nje. kwanza Dennis alipata mshituko na kisha akabaki akimkodolea macho baba yake bila kuongea neno na akiwa kasimama palepale mlangoni akiwa kama kapigwa na soti ya umeme. mzee Bisu naye alikuwa akimuangalia mwanaye kama kuna kitu alikuwa anasubiria kusikia kutoka kwake...
SASA ENDELEA NA SEHEMU YA 19
... Baba wewe si ulikwenda mazoezini?.." lilikuwa ni swali la kwanza la Denis mara tu baada ya kumsogelea baba yake.
:.. ndio si ndo nimetoka kwenye mazoezi yenyewe..." alijibu mzee Bisu huku akiendelea kumuangalia mwanae machoni. kama aliye kuwa anasubiria swali lifuatalo, na kweli lilikuwepo.
"... sasa umepita wapi, mbona mimi muda wote nilikuwa hapa sebuleni..." lilikuwa swali la pili la Dennis na alionekana mwenye mashaka sana usoni mwake.
mzee bisu naye alianza kupata wasiwasi akihisi kuwa mwanaye atakuwa kagundua kuwa alitokea chumbani kwa Hasina, lakini akajipa moyo baada ya kujishauri kuwa laiti mwanaye huyo angegundua kuwa alitoka chumbani asingemuuli maswali yale bali angemuuliza anatoka kufanya nini chumbani kwa Hasina, hivyo akajipa ujasiri na kuanza kujibu kwa kujiamini kidogo.
"... sasa wewe ilitaka nipite wapi?.."
"... nauliza hivyo kwa sababu mimi niko hapa muda mrefu..." aliendelea kuongea Dennis,
"... hebu nitolee maswali yako ya kipuuzi,.. mama yako yuko wapi sitaki kuchelewa chelewa tena leo..." aliamua kujifanya mkali ili Dennis asiendelee kumuhoji maswali, maana alishagundua kuwa mwanae huyo aliamua kudadisi ili kujua alikotokea. na kweli, Dennis alikuwa na masha lakini hakutambuwa ni wapi alikotokea baba yake. mara mlango wa chumba cha Hasina ukafunguliwa na Hasina akatoka na kuelekea jikoni. Dennis alimuangalia Hasina kisha akamgeukia baba yake, akilini mwake alikuwa akijiuliza kama inawezekana kuwa baba yake alitokea chumbani kwa Hasina, lakini wazo hilo akalitupilia mbali.
"... we Dennis, mi si nimekuuliza mama yako yuko wapi?.." alikurupushwa kutoka katika lindi la mawazo kwa swali hilo la mzee Bisu.
"... mama yuko chumbani kwake..." alijibu haraka haraka kisha akanyoosha na kuingia chumbani kwake.
mzee Bisu pia aliongoza moja moja chumbani kwake huku moyoni akijisemea "... nimeponea kwenye tundu la sindano... leo kama ningegundulika na mke wangu nilikuwa nimekwisha..." kule jikoni pia Hasina alihema kwa kwa nguvu baada ya kuona maswali ya baba na mwana yamekwisha, maana alipokuwa kule chumbani. alikuwa akiyasikia maswali waliyokuwa wakiulizana baba na mwana, na alikuwa tayari na wasiwasi akidhani kuwa Dennis atakuwa kagundua kuwa baba yake katokea chumbani kwake.
mzee Bisu alinogewa kweli na penzi la Hasina mtoto wa kitanga na ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani. alishaonja asali akaamua kabisa kujenga mzinga.
************************
Hasina alianza kuonekana msicha wa ukweli baada ya kuanza kupendeza kwa nguo alizonunuliwa na mzee Bisu, alionekana sister duh, ukilinganisha na umbo lake zuri basi alipendeza kwelikweli, jambo ambalo lilizidisha tamaa kwa mzee Bisu,.. pia chembe chembe za tamaa zilikuwa zikitembea mwilini mwa Dennis na akaanza kupiga mahesabu ya kumnasa Hasina ili aweze kupata naye utamu. lakini kwa Bi Pauline yeye alikuwa na maswali lukuki kulingana na mavazi ya Hasina, yamepatikana wapi? na hata kaka kanunua yeye, hela amezipata wapi? maana nguo zenyewe zilionekana ni za mbei kubwa hivyo akatamani sana kujua wapi alikopata nguo hizo, hata hivyo akaamua kukaa kimya lakini akilini mwake alishahisi kuwa hasina atakuwa na mwanaume ambaye ndo anayempatia pesa za kununulia hizo nguo, akapanga siku amuulize na kama ni kweli ana mwanaume, amrudishe kwao mapema ili asije akaleta mzigo wamimba pale nyumbani kwake.
ilikuwa ni jioni ya saa 10, Dennis alitoka kwenye mizunguuko yake na kurudi nyumbani, alipoingia ndani alikuta sebule ikiwa wazi yaani hakuna mtu, alisimama katikati ya sebule akaangalia huku na huku lakini hakuona mtu, akaongoza moja kwa moja chumbani kwake ambako hakukaa sana akatoka na kurudi kukaa sebuleni. Mara mlango wa chumba cha Hasina ukafunguka na Hasina akatokea akiwa katika vazi la kanga moja na huku mkononi akiwa kashikilia sabuni kwa lengo la kwenda bafuni kuoga, mwili wake ulionekana kulowa jasho, alipotokeza sebuleni alikutana macho kwa macho na Dennis, alishituka sana kumuona Dennis pale hadi dennis akagundua mshituko wake, hakumchelewesha akamtandika swali.
"... we vipi, mbona umeshituka kuniona?.."
Hasina hakujibu badala yake alianza kurudi nyumba kwa lengo la kurudi chumbani kwake. Dennis akaendelea kumuangalia kwa makini na akagundua kuwa kulikuwa na kitu kama uoga kwenye uso wake.
"... we Hasina, si nimekuuliza?.. mbona umeshituka na mbona uko hivyo?.. aliendelea kuhoji maswali na huku akiwa kamkazia macho.
"... hamna kitu ka... kaka Dennis..." alijibu Hasina huku akiwa tayari kasimama katikati ya mlango
"... sasa mbona umeshituka..."
"... hamna... si... si nilitaka kwenda kuoga..."
"...sasa kuna tatizo gani..."
"... hamna tatizo, lakini si... si nilijua hakuna mtu hapo sebuleni ndo maana nikashituka..." alijitahidi kunyoosha maelezo na huku akiwa tayari kakishika kitasa cha mlango
"... na mbona unatoka jasho hivyo kwani ulikuwa unafanya nini?.."
"... nilikuwa nimelala tu..."
"... sasa mbona umerudi nyuma wakati ulikuwa unaenda kuoga?.."
"... nachukua kanga nyingine..."
Dennis aliangalia huku na huku kisha akamuuliza
"... nani mwingine yuko hapa nyumbani?.."
"... niko mwenyewe... mama toka alivyoondoka ile asubuhi hajarudi mpaka saa hizi..." alijibu Hasina. jibu hilo ni kama lili mfurahisha kidogo Dennis akaamua kumuita
"... hebu njoo kwanza..."
"... ngoja nivae kanga nyingine..."
"...njoo hivyo hivyo..." aliongea Dennis. kuna kitu kilikuwa kinatembea kichwani kwa Dennis au labda niseme kuwa kuna kitu ambacho Dennis alishaanza kukitaka toka kwa Hasina.
"... ngoja nivae nguo kaka Dennis..."
Dennis akainuka na akawa kama anamfuta
".. au ngoja nije tukaongee kidogo chumbani kwako..."
Hasina alikurupuka pale mlangoni na kumkimbilia Dennis kisha akamzuia
"... haya basi nimekuja tuongee hapa hapa..."
Dennis akapatwa na mashaka, kidogo na akawa kama anajiuliza maswali mwenyewe..." huyu mbona nimezungumzia Habari za kuingia chumbani kwake tu amekurupuka wakati alikuwa hataki kunisogelea eti kwa vile kavaa kanga moja... au kuna kitu anaficha huko chumani nini?.."
KUNA NINI CHUMBANI KWA HASINA?...
USIKOSE SEHEMU YA 20
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.